23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa atoa wiki nne kuundwa Mabaraza ya Wafanyakazi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenyeulemavu, Jenista Mhagama kutoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu wa Wizara hiyo mpaka ifikapo Septemba 30, huu Mabaraza ya wafanyakazi katika Halmashauri yawe yameundwa.

Pia, amewataka waajiri wote nchini kupeleka michango ya wafanyakazi wao kwa wakati ambapo amedai pia ni jukumu lao kuwasafirisha wao, mizigo na familia zao pindi wanapostaafu.

Akizungumza leo Agosti 25, jijini Dodoma, wakati akifungua mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), ambao utaenda sambamba na uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Chama hicho watakaoongoza kwa miaka mitano.

Majaliwa amesema zipo baadhi ya Halmashauri ambazo bado hazijaunda Mabaraza ya wafanyakazi kutokana na sababu mbalimbali.

Kutokana na hali hiyo, amemweleleza Waziri Mhagama kuwaagiza Makatibu Wakuu wa Wizara hiyo kulisimamia jambo hilo ambapo amedai mpaka ifikapo Septemba 30, mwaka huu mabaraza hayo yawe yameundwa.

Aidha, amewataka waajiri wote nchini kulipa mafao kwa wakati ikiwa ni pamoja na anapostaafu mtumishi  kuhakikisha anasafirishwa mpaka nyumbani pamoja na mizigo na familia yake.

“Jukumu la mwajiri mfanyakazi wake anapostaafu ni kuhakikisha anarejeshwa nyumbani na mizigo yake,naagiza waajiri wote kupeleka michango kwa wakati,”amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kulipa madeni ya watumishi wa umma wanaostaafu  ambapo zaidi ya Sh bilioni 172.6 zimelipwa kwa walimu waliostaafu.

Amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kahakikisha inaendelea kuwa karibu na wafanyakazi nchini ambapo amedai wanaushirikiano wa kutosha na TALGWU katika utendaji kazi.

Kuhusiana na wanasiasa kuwaweka ndani wafanyakazi katika utendaji wa majukumu yao, Majaliwa amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na utoaji wa maagizo wanayoyatoa.

Vilevile, amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakipoteza haki zao kutokana na kutokuweka kumbukumbu ya mambo yao hivyo amewataka kufungua mafaili katika maeneo yao ya kazi ili iwe rahisi kutatua matatizo yao.

Kwa upande wake, Waziri Mhagama ameipongeza TALGWU kwa kufanya kazi kiweledi ambapo amedai  ni imara na wanafanya kazi kwa kuzingatia kanuni sheria na taratibu.

“Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni hawa wanafanya kazi nzuri nawapongeza sana. Nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri Mkuu Chama hichi ni imara  sana ndani ya nchi kama mlezi sioni aibu kusema kinafuata taratibu kanuni na sheria,”amesema.

Awali, akisoma risala, Katibu Mkuu wa TALGWU Taifa, Rashid Mtima amesema wanakabiliwa na changamoto za baadhi ya halmshauri kutokufanya vikao vya mabaraza,watumishi wanaostaafu kutokurudishwa nyumbani pamoja na kuleweshewa mafao,wanaotumia mapato ya ndani kutokulipwa kwa wakati katika bima na viongozi wa kisiasa kuwaweka ndani wakati wakitimiza wajibu wao.

“Tunaomba suala la upandishaji wa madaraja liangaliwe,tunaomba tupunguziwe kodi kwenye mishahara hii waliyopunguza ni ndogo,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles