31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Watanzania wahamasishwa kutembelea vivutio vya utalii

Na Sheila Katikula, Mwanza

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, ametoa wito kwa watanzania  kuweka utaratibu  wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo  nchini  na kuacha kuamini vivutio ni kwa ajili ya  wageni kutoka nje.

Wito huo umetolewa leo Alhamisi Februari 25, kwenye  kikao cha pili cha bodi ya barabara mkoa wa Mwanza kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika jijini Mwanza ambapo amesisitiza ni vvema kila mtu ahamasike kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga  za  wanyama na hifadhi za taifa. 

Amesema Watanzania wanapaswa kuwa wazalendo kwa kupenda  vivutio vyao na kuvitangaza kwani kuanzia mwaka 1993 kulikuwa na watalii waliokuwa wakiingia  kwenye hifadhi 230,000  na hadi kufikia mwaka 2019 idadi ya watalii iliongezeka na kufikia milioni 1.5 waliofanya utalii kwenye mbuga  mbalimbali zilizopo nchini.

” Watanzania tupo milioni 60 kwa sasa lakini ukiangalia idadi ya watu wanaoingia kwenye hifadhi zetu  na kuangalia utalii ni wachache kuliko  idadi ya watu waliopo nchini hali hii inaonyesha sisi siyo wazalendo ni  vvema tupende  utalii wa kwetu wa ndani.

“Tulikuwa tukitegemea sana watalii kutoka nje, kutokana na ugonjwa corona  walisita kuja lakini mwezi Desemba mahotel yote yalijaa  watu walijitokeza kutembelea mbuga zetu na kujionea wanyama waliopo.

“Kila mmoja anapaswa kuwa balozi wa kutangaza vivutio kwenye mtandano kupokea watalii kutoka ndani na nje  kwani kufanya hivyo kutapelekea kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Tunampango wa kuanzisha utalii wa majini  ambao utatumia ziwa victoria  kwa kutumia meli watakuwa wakitoka Serengeti watapita saa nane kwenda kisiwa cha lubondo watakuwa na uwezo wa kwenda  chato  itasaidia kutangaza hifadhi Buligi chato,” amesema Masanja.

Hata hivyo amesema kutokana  na   barabara kuchangia kwa asilimia kubwa   ongezeko la watalii nchini ni vvema wakala wa barabara  vijijini na mjini (TARURA) kuona umuhimu  kuzitengeneza ili kusaidia kupitika kwa ulahisi.

“Barabara zikiwa hazijatengenezwa vizuri inakuwa changamoto kupitika ni lazima wakala wa barabara vijijini na mjini (TARURA)  kuona  umuhimu wa kizitengeneza  na ikiwezekana kuongeza bajeti ili kusaidia kwenye matengenezo hayo, zitasaidia  kuvutia watalii na kufika eneo husika kwa urahisi na kwa wakati,”amesema Masanja.

 Kwa upande wake Kaimu Meneja Wakala la Barabara Vijijini na mjini  mkoa Mwanza, Mhandisi Mohamed Muada alisema  kutokana na bajeti iliyotolewa watahakikisha wanarekebisha  barabara  hizo kwenye maeneo korofi ili zisaidie kutangaza utalii nchini.

Naye Mwenyekiti wa  kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emanuel Kipole amewataka wajumbe hao kutekeleza kwa wakati  mambo yaliyo ndani ya uwezo wao kwani  kufanya hivyo kutasaidia kufikie malengo na kuleta maendeleo kwa wananchi kwenye maeneo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles