24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli aweka jiwe la msingi soko la kisasa Kisutu

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, amezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye Soko la kisasa la Kisutu lenye majengo ya Gorofa nne ambalo Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 13.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo leo Alhamis Februari 25, Rais Dk. Magufuli amesema soko hilo litakuwa na Vizimba zaidi ya 500 na Lina uwezo wa kupokea wafanyabiashara 1,500 ambapo ndani yake kutakuwa na Eneo la Machinjio, Sehemu za Mama lishe na Baba lishe, sehemu za kuuza nyama, huduma za kifedha Kama Bank, Maegesho, Ofisi na huduma zote muhimu.

Aidha Rais Dk. Magufuli amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha Ujenzi kabla ya March 17 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa TAMISEMI Ujenzi umefikia asilimia 95.

Hata hivyo, amesema uwepo wa masoko ya kutosha nchini yatawezesha wakulima kuwa na sehemu ya uhakika ya kuuza mazao yao Jambo litakaloinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amemshukuru Rais Magufuli kwa Mageuzi makubwa aliyofanya kwenye sekta ya Afya jijini humo ambapo amefanikiwa kuongeza Hospital za Wilaya kutoka 7 mwaka 2015 Hadi kufikia 11 sasa, Vituo vya Afya 8 mwaka 2015 adi kufikia 20 na ujenzi wa Zahanati kutoka 94 adi kufikia 121.

Aidha, Kunenge amesema Tayari Rais ametoa pia kiasi ch Sh Trilioni 1.62 kwa ajili ya maboresho ya huduma za umeme ikiwemo upanuzi wa vituo 24 na kufikisha umeme maeneo yaliyokuwa hayajafikiwa.

Pamoja na hayo Kunenge amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa Vyombo vya Usalama vinafanya kazi usiku na Mchana kuhakikisha Jiji kinaendelea kuwa shwari wakati wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles