25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Watanzania 10 kufanya kazi StarTimes China

1-4Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

WATANZANIA 10 wamepatikana katika shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoandaliwa na Kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China hapa nchini.

Washindi hao wamepata fursa ya ajira kwa kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing.

Akizungumza baada ya shindano hilo, Hilda Malecela, ambaye ndiye aliyeongoza kwa kupata alama nyingi kutoka kwa majaji, alisema anashukuru sana kupata fursa hiyo ya kuonyesha kila kipaji alichonacho kwani haikuwa kazi rahisi.

“Kwanza kabisa nashukuru kwa ushindi huu, haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa ukizingatia washiriki walioingia hatua ya fainali wote walikuwa wana uwezo mkubwa sana.

“Nawashukuru majaji kwa kunipa moyo tangu awali na hatimaye kuniamini kwamba nina kitu ambacho ninaweza kukitoa kwa Watanzania kupitia kipaji change cha sauti. Fursa niliyoipata pamoja na washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia na kuitumia ipasavyo.

“Napenda kuwaahidi Watanzania kuwa nitaitumia nafasi hii vema kuhakikisha nafanya kazi nzuri ili wao waendelea kuburudika na kujifunza zaidi kupitia filamu na tamthiliya. Nawapongeza pia StarTimes kwa kutambua umuhimu wa Kiswahili na kuja ubunifu huu ambao haujawahi kutokea nchini,” alisema Hilda.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao, alisema wamefurahia kampuni yao kuwa ni sehemu ya kukuza ajira nchini kwa kuwapata washindi hao ambao watafanya kazi chini ya StarTimes China.

“Hatukutegemea kama Watanzania wengi wangevutiwa na shindano hili lakini imekuwa ni kinyume chake kwani imedhihirika kuwa wapo wasanii wengi sana wenye vipaji vya sauti ,” alisema Liao.

Washindi kumi waliopatikana ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed, Sadiq Kututwa, Mathew Mgeni, Maisala Abdul, Rukia Hamdan, Richard Rusasa, Happiness Nyamayao, Jamila Hassan na Abraham Richard ambao wote wanakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles