Wataka wanaoishi kwenye hifadhi kukamatwa

0
381

Mohamed Hamad

Wananchi wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wameitaka Serikali kuwakamata wafugaji wanaoendesha maisha yao kwenye hifadhi ya jamii ya Emboley Murtangos kwa kufuga na kulima jambo ambalo haliruhusiwi.

Mahakama ya wilayani humo iliamurupasifanyike shughuli zozote za Kibinadamu katika eneo hilo la hifadhi kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa na mkulima Titu Shumo na wenzake 49 dhidi ya Serikali.

Kesi hiyo ilitokana na mvutano wa wakulima na wafugaji kugombea eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 133,333 ambalo lilisababisha maafa makubwa ya wakulima na wafugaji wakigombea ardhi.

Awali vijiji saba  kwa pamoja vilitenga eneo hilo kama hifadhi ya msitu ili waje kunufaika lakini baadaye ilionekana kuwa wanaonufaika ni upande mmoja jambo ambalo lilifanya kila mmoja kuvamia na kufanya shughuli za kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona mbele ya Mkuu wa Wilaya, Tumaini Magessa na Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Kiteto, Joakim Mwakiyolo alisema hataweza kutoa fedha kwaajili ya kuwaondoa waliovamia.

“Halmashauri tunaidai Serikali kuu bilioni moja tuliyoitumia kuwaondoa wavamizi wakati ulena swala hili lilisababisha watangulizi wangu kupata matatizo walipelekwa mahakamani, sasa siko tayari sitoi hata shilingi ya kuwaondoa waliovamia,” amesema Kambona.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, amethibitisha kuwa pamoja na amri ya mahakama kutolewa wakati huo na kutekelezwa, baadhi ya watu tena wamevamia na wanaendeleza shughuli za Kibinadamu kinyume cha sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here