25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Membe: nimefurahi kupata nafasi ya kufafanua mambo…

Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema amekuwa mtu wa furaha baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dodoma leo Alhamisi Februari 6.

Membe amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika mahojiano hayo yaliyochukua saa tatu.

“Tulikuwa na mkutano wa masaa matatu ya mijadala mizuri, mikubwa, ya kitaifa inayohusu Chama chetu Cha Mapinduzi na nchi yetu, na nimekuwa mtu wa furaha kubwa ajabu kwa sababu nimepata nafasi nzuri ya kufafanua mambo kadhaa ambayo chama changu ilitaka kuyajua.

“Nimepata nafasi ya kutoa mawazo ya yale mambo ambayo niliombwa kutoa, kwa hiyo sasa hivi mimi na mke wangu tunakwenda kula chakula kizuri sana kwenye hoteli moja ambayo haijulikani baada ya hapo nitaanza safari ya kurudi Dar es Salaam, lakini niwaambie safari hii ya kuja Dodoma, ilikuwa ni ya masaa makubwa sasa sana kwa kwa chama na kwa taifa…” amesema Membe.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles