24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wamwangukia Lipumba

 AMINA OMARI

WANANCHI visiwani Pemba wamwangukia Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na kusema watamuunga mkono wakati wa uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Lakini pia wananchi hao, walisema maeneo yote ya visiwani humo, ni ngome ya chama hicho hawapo tayari kwenda kumuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharifu Hamad.

Wananchi hao, waliyasema hayo juzi, wakati Profesa Lipumba alipokuwa kwenye ziara yake visiwani Pemba,

Walisema wana kila sababu ya kukiunga mkono chama hicho, licha ya kuyumbishwa na Maalim Seif,baada ya kukihama chama hicho.

Mmoja wa wazee,Juma Haji alisema Maalim Seif anapaswa kutambua chama cha CUF hakitokufa, badala yake kitasonga mbele kwa maendeleo ya wananchi.

Baadhi ya wananchi wengine wamesema hawana imani na Maalim Seif, kwani tokea patokee migogoro baina yake na chama hakufika na kuzungumza nao juu ya mwenendo wa chama alichohamia cha ACT Wazalendo.

‘’Huku ni ngome ya CUF, hatuwezi kubadilisha hili sisi hatuwezi kuiacha huo ndiyo ukweli na tunakila sababu ya kukienzi chama chetu kwani ni chama kunachosimamia sera na haki sawa kwa wananchi wote hatuwezi kwenda ACT miaka yote walikuwa wapi walihoji wananchi hao.

Akizungumza na wananchi hao wa micheweni Profesa Lipumba, alionyesha kufurahishwa na mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa wananachi hao na kuwatoa hofu juu ya chama chao kuwa bado kipo ngangari.

Alisema chama hicho ni cha haki sawa kwa wrote kuanzia haki za kiuchumi, kijamii na hata kisiasa ambapo amewataka wajipange katika uchaguzi mkuu kuhakikisha serikali ya umoja wa kimataifa kinashirik kikamilifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles