25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 23, 2021

Biteko asifu mkakati uwekezaji wa GGML

 MWANDISHI WETU – GEITA 

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko ameipongeza Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu – Geita (GGML) kwa kuwa mdau wa mfano katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Geita. 

Biteko ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika ziara fupi aliyoifanya mkoani Geita na kukagua miradi inayotekelezwa na Kampuni ya GGML chini ya mpango wake wa kusaidia jamii katika Mji wa Geita. 

Alisema lengo la Serikali ni kuona maisha ya watu katika maeneo yote yenye rasilimali madini, ikiwemo Geita yanabadilika kiuchumi. 

“Nimefurahishwa na namna ambavyo Serikali katika Mkoa wa Geita inavyosimamia ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye sekta ya madini. Tayari tumeshafikia lengo la kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 400 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 kutoka kwenye sekta hii, na sehemu kubwa ya makusanyo haya imetoka Geita, hususan GGML. 

“Inatia moyo sana kuona kwamba sekta hii sasa inachangia zaidi ya asilimia 5 ya uchumi wa nchi yetu. Lengo ni kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025,’’ alisema Biteko.

 Mojawapo ya miradi ambayo ilikaguliwa na waziri huyo katika ziara yake ni ujenzi wa Kanda maalumu ya uwekezaji ambao utasimamiwa na Mamlaka ya ukanda maalumu wa Uwekezaji (EPZA) na Halmashauri ya Mji wa Geita. 

Pia alitembelea miradi mingine ya kimkakati inayofadhiliwa na GGML, ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu la Geita Mjini na soko la Katundu. 

Aidha, Makamu wa Rais anayeshughulikia Maendeleo Endelevu katika Kampuni ya GGML, Simon Shayo alisema utekelezaji wa miradi ambayo imetembelewa na waziri Biteko ni sehemu ya mpango wa mwaka 2018/19 unaoenda sambamba na mojawapo ya tunu za kampuni hiyo inayoelekeza kwamba jamii inayozunguka shughuli zake sharti ifaidike kwa uwepo wake. 

Alisema GGML ambayo ni sawa na kampuni-raia inawajibika ipasavyo kwa jamii kwani hutumia Sh bilioni 9.2 kila mwaka kugharimia miradi ya jamii katika mkoa wa Geita na kuifanya kampuni hiyo kuwa ya kipekee kutokana na mchango mkubwa inayotoa kusaidia jamii. 

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,794FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles