24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Kuweni macho

 MWANDISHI WETU– DODOMA

RAIS Dk. John Magufuli amewataka Watanzania kuwa macho na makini dhidi ya mbinu zozote zinazoweza kufanywa kuwaambukiza ugonjwa wa corona ama magonjwa mengine.

Pia aliwashukuru viongozi wa dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mungu ili aepushe janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona. 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilisema Rais Dk. Magufuli alitoa shukrani hizo jana alipokaribishwa kuwasalimu waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Chamwino mkoani Dodoma baada ya kuhudhuria misa takatifu ya Sikukuu ya Utatu Mtakatifu.

Misa hiyo, iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padre Paulo Mapalala.

Taarifa hiyo, ilisema Rais Magufuli alisema Mwenyezi Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake nikuwa maambukizi ya virusi vya corona yamepungua na wananchi wanaendelea na maisha yao, huku wakichapa kazi za uzalishaji mali, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ugonjwa huo ungesababisha madhara makubwa.

 Alitoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa makini dhidi ya mbinu zozote zinazoweza kufanywa kuwaambukiza ugonjwa huo ama magonjwa mengine, huku wakimshukuru na kumtumaini Mwenyezi Mungu aliye muweza wa yote.

Akiwa Kanisani hapo, Rais Magufuli aliendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha Sh milioni 17,229,000 (ikiwemo shilingi milioni 10 aliyochangia yeye mwenyewe) na mifuko 76 ya saruji, na ametaka upanuzi wa kanisa hilo uanze leo.

Tangu kuibuka kwa corona, Rais Dk. Magufuli aliwahimiza Watanzania kumuomba Mungu, huku wakifanya kazi bila hofu.

Kwa mara ya kwanza, aliwaomba viongozi wa dini na Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu wakati ugonjwa umeingia kwa kasi, jambo ambalo lilitekelezwa kwa ufasaha.

Pia, baada ya wagonjwa kupungua katika hospitali mbalimbali, Rais Magufuli aliwaomba Watanzania kumshukuru Mungu kwa kusaidia kupungua maambukizi ya ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles