24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Robanda waondokana na kero ya maji

Na Malima Lubasha, Serengeti

UGUMU katika upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Kijiji cha Robanda Kata ya Ikoma wilayani Serengeti mkoani Mara umetatuliwa baada ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) kukamilisha maboresho ya miundo mbinu ya mradi wa maji Robanda.

Awali, wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakilalamika kutumia muda mwingi kutafuta maji visimani na hata kutumia fedha nyingi kununua maji ambayo siyo salama kwa afya.

Akizungumzia hali ya huduma ya maji, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Serengeti, Mhandisi Deus Mchele, alisema kuwa kwa sasa wanaridhishwa na upatikanaji wa maji kijijini na kuwataka wananchi kujitokeza kuunganishiwa maji huku uongozi wa kijiji ukitakiwa kusimamia suala la kulipia umeme kusukuma maji.

“Tumefanya kikao na uongozi kujadili mambo mbalimbali kuhusu uendeshaji wa mradi huo wa maji katika kijiji cha Robanda ikiwamo kuunda upya kamati ya uendeshaji mradi mbali na kujitokeza changamoto ndogo ndogo tunashukuru hivi sasa wananchi wameanza kupata maji safi na salama,” amesema.

“Tulihitaji huduma hii iwafikiye wananchi, sasa hata shughuli za maendeleo na miradi midogo midogo ya binafsi zitakwenda kwa kasi, ni wakati wetu sasa tujitokeze kuunganishiwa huduma ya maji ili yafike kwe nye nyumba zetu,” amesema Mchele.

Mkazi wa kijiji hicho, Kenyata Mosoka alisema kuwa kwa muda mrefu walikuwa na kero katika kupata ma ji safi na salama,hivyo ujio wa mradi huo ni ukombozi kwao.

“Kila mtu anajua huduma ya maji katika kijiji hicho ilikuwa ni ndoto, zilianza habari tu wengi hatuamini kwamba ipo siku tutapata maji ya bomba ila RUWASA wametekeleza mradi huu na sasa tunapata maji safi na salama ingawa zipo changamoto ndogo ndogo, tunawapongeza sana na kuahidi kutoa ushirikiano katika ulipaji wa huduma hii,” alisema Mosoka.

Msimamizi wa mradi huo kutoka RUWASA, Michael Mauka alisema kwa sasa tunaendelea kukamilisha changamoto ndogondogo zilizopo katika vituo 17 vya kuchotea maji ambavyo vipo vizuri hivyo wananchi wajitokeze kuunganishiwa huduma ya maji.

“Tumeanza kuunganisha huduma ya maji kwenye mradi huu wa maji Robanda ambao uko katika hatua nzuri chanzo chake ni kisima kirefu umbali wa kilometa 7 toka hapo hadi kijijini palipo na tanki lenye ujanzo lita laki tano baada ya mashine mpya kusimikwa kusukuma maji iliyokuwa changamoto kubwa,” amesema Mauka.

Mradi wa maji Robanda ulioanza mwaka 2021 una thamani ya Sh milioni 600 umekamilika ambao umewaondolea adha wakazi wa kijiji hicho chenye kaya zaidi ya 500 wananufaika kupata maji karibu na nyumba zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles