29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Wakatoliki kusali jumamosi

Askofu-Severin-NiwemugiziUPENDO MOSHA NA NORA DAMIAN

BAADHI ya Majimbo ya Kanisa Katoliki nchini, yametoa ruhusa maalum kwa mapadri yakiwataka kuendesha ibada zao siku ya Jumamosi ya Oktoba 24 badala ya Jumapili mwaka huu ili kutoa nafasi kwa waamini wao kushiriki Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani kwa uhuru.

Hatua hiyo inatokana na siku ya Jumapili ambayo waamini wengi wa kanisa hilo huabudu kuangukia Oktoba 25 ambayo ni siku ya Uchaguzi Mkuu.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata mjini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, zinasema kila askofu wa jimbo ana mamlaka ya kutoa maelekezo ya aina hiyo kwa waamini wake.

Askofu Niwemugizi alisema kila askofu katika jimbo lake anawajibika kufanya hivyo, kwani ni haki ya msingi ya waamini wake kupiga kura.

“Kilitrujia siku ya bwana inaanza Jumamosi jioni, kwa msingi huo wanaweza pia kuadhimisha dominika bila tatizo lolote.
“Si utaratibu wa kawaida kwa sababu kama baraza hatujakaa, lakini kila askofu anawajibika ndani ya jimbo lake, hivyo anaweza kutoa fursa hiyo. “Hata mimi katika jimbo langu la Rulenge Ngara, nimetoa kibali hicho kwa makanisa yote… kwa wanaotaka wala siwalazimishi wote,” alisema Katika hatua nyingine, askofu huyo alizungumzia mwenendo wa kampeni za uchaguzi, alisema amesikitishwa na dharau na matusi yanayotolewa na wanasiasa katika
majukwa ya kampeni.

“Kumekuwa na lugha chafu, hakuna anayeona kama amefanya vibaya kwa mwenzake,…. kwa mfano unamwita mwenzako oil chafu, maana yake unamdharau muumba aliyemuumba hata kama ana upungufu.

Alisema tabia hiyo ya kutoleana lugha chafu ipo siku viongozi wa dini nao wategeukiwa.

MOSHI

Habari kutoka Jimbo Katoliki la Moshi mkoani Kilimanjaro na Mbulu mkoani Manyara, zinasema kanisa hilo limetoa ruhusa maalumu kwa waamini wa majimbo hayo kusali ibada ya Jumapili Oktoba 24, ili kutoa fursa kwa waamini hao kwenda kupiga kura.

Uamuzi huo unatokana na waraka wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Isaac Amani uliosambazwa katika makanisa yote ya majimbo hayo.

Waraka huo wenye kumbukumbu namba PROT Na. BSH/2657/2015- VIII/B kwenda kwa mapdre, watawa na waamini walei, uliosainiwa na Askofu Aman unawahimiza waamini wake kushiriki Uchaguzi Mkuu.

“Wakati kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiendelea, ni muhimu wananchi wafuatilie hotuba za wagombea ili hatimaye waweze kuchagua viongozi wenye sera na sifa za kuleta maendeleo ya wananchi.

“Tunaendelea kumwomba Mungu atujalie amani wakati wa kampeni, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi wagombea na wananchi wayapokee matokeo kwa utulivu na raha ya kudumisha umoja na amani ya kitaifa.

“Kwa kuwa siku ya uchaguzi ni Dominika, nawaletea tangazo la kuboresha mazingira ya kupiga kura. Kwa waraka huu natoa kibali maalumu kwa mapadre majimboni Mbulu, Moshi kufanya ibada ya Dominika ya 30 ya mwaka huu siku ya Jumamosi Oktoba 24.

“Lengo la kibali hiki ni kuwapa wapiga kura fursa ya kupata ibada Jumamosi jioni na Jumapili asubuhi ili wakapige kura mapema. Hata Mapadre wanatakiwa kushiriki zoezi hili la kitaifa. Kwa hiyo ratiba za misa zipangiliwe maparokiani na vigangoni kwa kuzingatia kibali kilichotolewa.

“Natumia fursa hii kuwahimiza wale wote waliojiandikisha watumie haki na wajibu wa kupiga kura ili tupate viongozi wazalendo tunaowapenda. Kura yako ni muhimu katika harakati za kuwasaka viongozi, madiwani,wabunge na rais.
“Usiachie wengine wakuchagulie viongozi wakati wewe unao wajibu wa kupiga kura. Ukishapiga kura yako rudi nyumbani ukangojee matokeo,”ilisema sehemu ya waraka huo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mhashamu Askofu Amani ambaye pia ni msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki la Mbulu alisema kutoa fursa hiyo ni kuwataka waamini wake kutumia haki ya kidemokrasia ya kupata viongozi.

Alisema ratiba za misa zote za ibada zitapangwa kwa parokia zote na vigango vyote kwa mujibu wa kibali kilichotolewa na kanisa hilo.
Uamuzi huo wa kanisa unakwenda sambamba na ushauri uliowahi kutolewa siku za nyuma na Jukwaa na Katiba Tanzania (JUKATA) pamoja na wadau wengine. Wadau hao waliwahi kupendekeza kuhusu haja ya siku ya Uchaguzi
Mkuu ibadilishwe ili kutoa fursa kwa waamini ya dini ya Kikristu kutumia vizuri haki yao ya kupiga kura, ili siku ya jumapili waitumie kwa ajili ya ibada tu.

Utaratibu huo wa siku maalum ya kupiga kura ulitumiwa na nchi ya Kenya katika uchaguzi mkuu uliopita, uliomuweka madarakani Rais Uhuru Kenyatta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles