27.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

WAJASIARIAMALI WASHAURIWA KUJIUNGA NA VIKUNDI

Patricia Kimelemeta, Kimelemeta


Wajasiriamali wadogo na wa kati wameshauriwa kujiunga na vikundi mbalimbali nchini ambavyo vitawasaidia kupata mikopo kwa ajili ya kuboresha biashara zao.

Hayo yalisemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBA Emeke Lweirebor ya jijini Dar es Salaam ambaye amesema kuwa wajasiriamali ni injini ya kukuza uchumi wa nchi, hivyo kujiunga kwenye vikundi hivyo kutawasaidia kupewa fedha za mikopo ambazo zikitumika vizuri zitaboresha shughuli zao pamoja na kukuza mtaji.

“Katika nchi zote za Bara la Afrika au nje ya Bara hili,wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa wanaheshimika sana kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi, hivyo kila benki ikiwamo UBA itahakikisha inawapa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji ya biashara zao, jambo ambalo linaweza kukuza uchumi,” alisema Emeke.

Lweirebor liongeza kuwa fursa iliyopo ni kuhakikisha wana panga Mipango yao ambayo itawasaidia kupata fedha na kutekeleza maazimio yao.

Aidha Emeke alisema benki hiyo inashirikiana na serikali kwenye mkakati wa kuanzisha viwanda ili kuhakikisha vinafanya kazi ya kutoa ajira kwa wananchi na kuzalisha bidhaa bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles