27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

HALMASHAURI ZA LINDI ZAPEWA BENDERA NYESI KWA KUWA YA MWISHO KITAIFA.

Na Hadija Omary, Lindi


Halmashauri za wilaya ya Ruangwa, Lindi vijijini ,Kilwa na Liwale mkoani Lindi zimepewa bendera nyeusi ikiwa ni zawadi ya kufanya vibaya na kupelekea kuwa ya wa mwisho kimkoa katika mitihani mbali mbali ya upimaji kitaifa.

Upataji wa zawadi ya bendera hizo nyeusi ambazo zinatakiwa kupepea kwa kipindi cha mwaka mzima katika Halmashauri hizo ni miongoni mwa maadhimio ya mikutano na vikao mbali mbali vya elimu vilivyoketiwa mkoani hapo vya namna ya kupandisha ufaulu wa mitihani katika mkoa wa Lindi.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa elimu mkoa wa Lindi Wengi Mchuchuli alisema Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imepata bendera nyeusi kwa kuwa ya wisho katika mtihani wa  kumaliza elimu ya msingi, Lindi Vijijini kwa kuwa ya mwisho katika mtihani wa darasa la nne, Halmashauri ya Liwale kuwa wa mwisho katika mtihani wakidato cha pili na Ruangwa kwa kuwa wa mwisho katika mtihani wa kidato cha nne.

Mchuchuli alisema lengo la kuweka utaratibu huo ni kutaka kupandisha kiwango cha ufaulu katika mkoa huo kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia waliofanya vizuri waendelee kufanya vizuri zaidi  na waliofanya vibaya wafanye vizuri ili kukwepa bendera hizo nyeusi ambazo zinaonekana kuharibu sura ya Halmashauri zao.

Akizungumza katika mkutano wa juma la elimu uliofanyika juzi ukumbi wa kagwa Manispaa ya Lindi uliokutanisha wadau mbalimbali wa elimu Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi alisema utaratibu huo utakuwa endelevu kwa Mkoa wa Lindi na kwamba bendera hizo zitakuwa zinazunguka Wilaya na Wilaya kwa kadri ya matokeo ya mitihani ya upimaji wa kitaifa yatakapo tangazwa na

Ndemanga pia alitoa wito kwa Halmashauri zote za Mkoa wa lindi ambazo hazijatekeleza azimio la mkutano mkuu wa Wadau wa elimu la kutoa zawadi kwa walimu na shule zilizofanya vizuri katika Halmashauri kufanya hivyo mara moja na kuwapa muda wa siku 21 zoezi hilo liwe limekamilika

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles