KABUDI: MAZUNGUMZO KUHUSU MAKINIKIA KUMALIZIKA MWEZI HUU

0
1634

Maregesi Paul, Dodoma          |              


Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema mazungumzo kati ya serikali na Kampuni ya Barrick yanaendelea vizuri na yanaweza kumalizika kati ya mwezi huu na mwezi ujao.

Profesa kabudi ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo, alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha wa 2018/19.

“Ili kuhakikisha sekta ya madini inawanufaisha Watanzania, serikali inafanya mazungumzo na kampuni nyingine za uchimbaji wa madini zikiwamo kampuni 10 zinazojihusisha na biashara ya madini ya Tanzanite.

“Aidha, Kampuni ya Tanzanie One ambayo imeshaanza mazungumzo na serikali imekubali kuilipa fidia serikali kutokana na ufanyaji wake wa biashara nchini na pia kampuni hiyo imekubali kulipa tozo na kodi zote inazotakiwa kulipa,” amesema Profesa Kabudi.

Hata hivyo, Profesa kabudi hakutaja kiasi cha fedha kilicholipwa na Kampuni ya Tanzanite One kwa kile alichosema watu wanaoidai serikali wanaweza kuanza kuidai serikali madeni yao.

Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi kwamba serikali imejipanga kutetea sekta ya madini ili rasilimali hiyo iwanufaishe Watanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here