26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Waganga tiba asili Bariadi wapewa siku 16 kuwa na vitambulisho vya JPM

Derick Milton, Simiyu

Waganga wa tiba asili waliopo wilayani humo, wamepewa siku 16 kuhakikisha kila mmoja anakuwa na kitambulisho cha wajasiriamali kilichotolewa na Rais John Magufuli.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya hiyo Festo Kiswaga wakati akiongea na viongozi wa waganga hao mkoa, alipokutana nao kujadili namna bora ya kuboresha kazi zao.

Kiswaga amesema kuwa katika wilaya hiyo kuna waganga wa tiba asili 600, na kwamba mganga yeyote ambaye hatakuwa na kitambulisho hicho baada ya siku hizo kuisha atafutiwa leseni yake na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Hadi kufikia Februari 20, mwaka huu kila mganga wa jadi awe na kitambulisho hicho, usipokuwa nacho tutakunyang’anya leseni yako kukuzuia kuendelea kufanya kazi zako, baada ya muda huo,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waganga hao, Samson Maduhu amesema ndani ya muda huo waganga wote 600 wanafikiwa na kupatiwa vitambulisho hivyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles