27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Messi hatarini kuikosa Real Madrid Jumatano

KATALUNYA, HISPANIA

KOCHA wa Barcelona, Ernesto Valverde, amesema mshambuliaji wake, Lionel Messi, anahitaji uchunguzi wa kina kabla ya kuvaana na Real Madrid katika mchezo wa Copa del Rey utakaochezwa Jumatano hii katika Uwanja wa Camp Nou, Hispania.

Messi juzi alipata jeraha la mguu na kutolewa nje ya uwanja kipindi cha pili  dhidi ya Valencia.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Hispania uliochezwa Uwanja wa Camp Nou, timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2.

Barcelona na Real Madrid zitacheza mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali  ya michuano ya Copa del Rey Jumatano hii katika Uwanja wa Camp Nou, hivyo kama jeraha la Messi likiwa kubwa huenda akaukosa mchezo huo.

Timu hizo pia zitacheza mchezo wa marudio Uwanja wa Bernabeu Februari 26 mwaka huu.

Katika mchezo dhidi ya Valencia,   mabao yote ya Barcelona yalifungwa na  Messi dakika ya 39 kwa mkwaju wa penalti na bao la pili akilifunga dakika ya 64, wakati yale ya Valencia yakifungwa na Kevin Gameiro dakika ya 24  na  Daniel Parejo dakika ya 32.

Valverde alithibitisha kuwa  Messi  alipatwa na tatizo katika mchezo huo,  hivyo watalazimika  kusubiri majibu ya uchunguzi ndipo wafahamu kama atakuwapo katika kikosi kitakachocheza dhidi ya Real Madrid.

“Messi amepatwa na tatizo kidogo,” alisema Valverde baada ya mechi kumalizika. “Hatufahamu kakutwa na kitu gani, tunatakiwa kusubiri hadi hapo tutakapopewa taarifa ya uchunguzi, kama  yataonyesha kuwa hana tatizo basi tutamtumia. ”

Akizungumzia mchezo dhidi ya Valencia, kiungo wa Barcelona, Ivan Rakitic, alisema ulikuwa mchezo mzuri, lakini alisikitika kutokana na matokeo ya sare waliyopata.

“Tulikuwa na hamu ya kubadili matokeo,” alisema Rakitic. “Katika kipindi cha pili tulikuwa katika kiwango bora, ilionekana mpira ulikuwa upande wetu, lakini tulikosa kutumia vema nafasi tulizotengeneza.”

Matokeo hayo yanaifanya Barcelona kuongoza Ligi Kuu Hispania ikiwa na  tofauti ya pointi sita dhidi ya Atletico Madrid, ambayo ipo nafasi ya pili na pointi 11 dhidi ya Real Madrid, ambayo ipo nafasi ya tatu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles