24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Hivi Sarri anawafahamu vizuri wachezaji wa Chelsea?

ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

TIMU ya Chelsea ilianza msimu huu wa Ligi Kuu England kwa ushindi mfululizo na kufanya wasifungwe hadi ilipofika Novemba mwaka jana.

Ushindi huo ulifanya kuwapo kwa majadiliano mengi kuhusu adithi nzuri inayimuhusu  Maurizio Sarri na  mtindo wake wa ufundishaji  uliompa mafanikio katika klabu yake ya awali ya Napoli.

Katika wiki  za mwanzo Jorge Luiz Frello Filho ‘Jorginho’ alijiunga na  klabu hiyo na kuanza kibarua chake kama kiungo mchezesha wa timu hiyo akitokea chini wakati  N’Golo Kanté, akionekana kufurahia jukumu lake jipya akicheza kama winga baada ya kuondolewa kuwa kiungo mkabaji.

Lakini  mabadiliko hayo yameanza kuwa na athari hasi kwa Sarri na inaonekana kama furaha ya mashabiki ya kumpokea mgeni huyo imemalizika pale Chelsea.

Kwa sasa kiwango cha timu hiyo kimepungua na kitendo cha kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal wiki mbili  zilizopita  kilifanya kupoteza michezo minne kati ya 11  ya Ligi Kuu England.

Mbali na  hayo yote kutokea lakini kitu cha kushangaza ni kitendo cha Sarri kuwavaa na kwashutumu wachezaji wake  kwa kushindwa kuelewa mfumo wake akitumia kauli mbalimbali pengine za kuudhi kwa wachezaji.

Sarri anasema:“Nataka kuwa mkweli kwao nikiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo na wakati mwingine hata  hadharani.”

Hii ni kauli ya Sarri baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu England ambao Chelsea ilifungwa mabao 4-0 dhidi ya  Bournemouth wiki iliyopita, kichapo ambacho kilimfanya kocha huyo kujifungia katika vyumba vya kubadilishia nguo na wachezaji hao.

Uamuzi wa Sarri kuamua kuishi katika njia hiyo  inaweza kuwa hatari anayoitengeneza hasa  kwa kuwa bado mgeni pale Chelsea.

Kitecho chake cha kuwapinga wachezaji hadharani kinaweza kuwa na matokeo  mawili:Wachezaji wanaweza kutaka kumuonyesha  kwamba wanaweza kumudu vema mfumo wake wa ‘Sarri-ball’ tofauti anavyofikiria au kikosi hicho ndio kikapotea kabisa.

Sarri anatakiwa kumalizana na vijana wake wakiwa faragha kwenye vyumba vya kubalishia nguo lakini si kuwasema ovyo hadharani.

Kitendo anachofanya Sarri sasa kilionekana hivi karibuni katika klabu ya Manchester United wakati ikiwa chini ya kocha Jose Mourinho, dhidi ya wachezaji kama Marcus Rashford, Luke Shaw na Paul Pogba.

Kwa kawaida wachezaji huwa katika presha ya kutosha ya kufanya vema mbele ya mashabiki  na vyombo vya habari bila kocha kuweka matatizo ya wachezaji  wake hadharani.

Wachezaji wakubwa katika timu hawataruhusu jambo hilo litokee na kuwaathiri kwa kuwa si matokeo ambayo wakati mwingine wanayataka.

Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson, amekuwa mmojawapo wa makocha wakubwa wa wakati wote, alikuwa na utawala wa dhahabu usiopingana na wachezaji wake hadharani licha ya kuwa anajulikana sana kuwa mwenye hasira  wakati anapochukia jambo fulani akiwa ndani ya vyumba vya kubadili nguo.

Ferguson alitumia njia hii kuwalinda wachezaji wake kwa  mashabiki na  ilimletea ufanisi usio wa kawaida na uaminifu kwa wachezaji wake.

Lakini makocha wengi wa kisasa huwa hawapendi kuitumia njia hii.Bado sababu za kushindwa huko hazijawa wazi.

Kwa Sarri  kuitumia njia hii Chelsea ni jambo la kushangaza.Chelsea imekuwa kati ya timu tatu za juu zenye nguvu katika Ligi Kuu England kwa misimu minne iliyopita:Ilipokuwa chini ya Mourinho, Antonio Conte na sasa Sarri.
Kati ya hao makocha, Mourinho hatimaye aliondoka baada ya wachezaji kuchoshwa  na tabia yake dhidi yao kama ilivyokuwa kwa Conte licha ya mafanikio ya haraka aliyoyapata akiwa na kikosi hicho.
Hii ndio hali ambayo Sarri anaweza kuipitia majira ya joto na anatakiwa kwenda nayo kwa uangalifu sana au inaweza kummaliza vibaya kama ilivyotokea kwa watangulizi wake.

Wote Mourinho na Conte waliondoka lakini walitwaa taji la Ligi Kuu kabla uhusiano wao na wachezaji kutofautiana.

Katika kipindi hiki kigumu, Chelsea tayari imemsajili kwa mkopo mshambuliaji, Gonzalo Higuin, kutoka Juventus.

Raia huyo wa Argentina amefunga mabao mengi wakati akiwa chini ya Sarri katika kikosi cha Napoli na inatarajiwa kufanya sawa kama alivyokuwa wakati huo.

Ujio wake unafanya  Eden Hazard abadilishwe nafasi ambayo alikuwa akichweza kama namba tisa ya uongo.

Mbelgiji  huyo alionekana kuifurahia nafasi yake  ambayo inamfanya mara nyiki awe na mpira  lakini kwa sasa atakuwa akitokea kushoto.

Inawezekana ujio wa Higuain ukawa nafuu kwa Sarri, lakini labda ukawa ishara nyingine kukamilika kwa mwisho wa Mtaliano huyo ambaye ameshindwa kubadilika kimfumo na mbinu.
Ujio wa Higuain unamaanisha Sarri   anapenda kutumia njia  ile ile kwa wachezaji wale wale.

Makocha wengi hupenda kusajili wachezaji ambao waliowahji kufanya nao kazi kwa mafanikio lakini hiyo haina maana kwamba wataendelea kufurahia mafanikio pamoja.

Jorginho alikuwa mchezaji wa kwanza kumfuata Sarri pale Chelsea akitokea klabu ya Napoli, na baada ya wiki chache alionekana kufanya mabadiliko ndani ya kikosi.
Lakini haikuchukua muda mrefu sana kwa timu pinzani kugundua kuwa zikiweza   kumfanya Jorginho hasicheze ndani ya uwanja ni sawa  na  kuisimamisha Chelsea isishambulie.
Jorginho, hana athari ambayo inaweza kuhalalisha kulazimisha Kanté kuondoka katika jukumu lake la kawaida.
Kanté ni injini ya timu ya Chelsea, kama alivyokuwa wakati timu hiyo iliponyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu na akiwa  katika klabu ya Leicester, bila kutaja upande wa timu ya taifa ya Ufaransa ambayo imenyakuwa Ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka jana nchini Urusi.
Ujio wa kocha mpya na mabadiliko ya nafasi  ya Kante ni sawa na kocha atakayechukua nafasi ya Mauricio Pochettino pale Tottenham na kumuhamisha mshambuliaji, Harry Kane, kucheza kama winga.
Kanté hajawahi kuzungumza juu ya mabadiliko yake na inawezakana akawa katika hisia kama alizonazo Hazard, kwa mfano, alipotakiwa kucheza kama namba tisa ya uongo na Conte lakini licha ya kuwa mtu mzuri, mwenye ujasiri bado ana athari kubwa kwenye timu hiyo.
Labda Sarri, aliyejulikana kwa  aina ya mtindo wake wa kushambulia, haoni kazi inayofanywa na Kanté.
Lakini kwa hakika Sarri anaweza kuangalia sifa za wachezaji kama vile Kanté na kucheza nao katika majukumu yao waliyozoea ambayo yamewafanya kuwa na mafanikio katika klabu ya Chelsea.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles