23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waepuka kero ya kupata elimu

UPENDO MOSHA, SIHA

SERIKALI wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, imesema changamoto iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa Kata ya Orkolili ya kutembea umbali mrefu kila siku kufuata elimu, imetatuliwa baada ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika Shule ya Sekondari Sinyari, kukamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu, alisema kukamilisha kwa ujenzi huo utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwa kuwa suala hilo lilikuwa likisababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu.

“Serikali kwa kushirikiana na wananchi, tumefanya jitihada za kumaliza ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ile na tunategemea Januari 7, mwaka 2019, wanafunzi waanze masomo.

“Kitendo cha wanafunzi wale kutembea umbali mrefu wa kilomita 24 kila siku kwenda masomoni katika shule ya sekondari Nuru na Sekirari, kilikuwa kinawaumiza watoto na kilichangia vijana wengi kukatisha masomo na kusababisha ufaulu kuporomoka katika wilaya yetu.

“Wanafunzi wanaofaulu katika shule za msingi Mkombozi na Orkolili zilizoko kwenye kata hiyo, wataanza masomo katika shule hiyo badala ya kwenda shule za sekondari Nuru au Sekirari.

“Pamoja na kukamilika kwa vyumba hivyo vya madarasa, pia miundombinu yote muhimu ikiwamo vyoo, vimekamilika pamoja na kwamba bado tuna mahitaji ya walimu, madawati na vitabu.

“Pamoja na hayo, wazazi wahakikishe wanawaleta watoto wao kupata elimu bora shuleni hapo kwa sababu tumejipanga kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya usomaji.

Mbali na hayo, mkuu huyo wa wilaya, aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule wanafunzi wote waliofaulu na waache tabia ya kuwakatisha masomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles