24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wachimbaji dhahabu wawili wafariki dunia kwa kufukiwa na kifusi

 Na Allan Vicent, Tabora

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo wakati wakichimba madini ya dhahabu katika kitongoji cha Maponda kijiji cha Igurubi kata ya Igurubi tarafa ya Igurubi wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Kaimu Mtendaji wa Kkata ya Igurubi, Godfrey David alitaja waliofariki kuwa ni Mrisho Luge (32) mkazi wa Mkoa wa Arusha na Mussa Cosmas (41) mkazi wa Masumbwe Mkoani Geita.

 Alisema tukio hilo limetokea leo Mei 26, 2021 saa 7 usiku wakati wachimbaji hao wakiwa katika mgodi huo ulioko katika Kitongoji cha Mapunda Namba 5 ambapo waliangukiwa na ukuta wa udongo wakiwa ndani ya shimo na kufariki papo hapo.

Amebainisha kuwa baada ya kupata taarifa hiyo walienda eneo la tukio na kufanya juhudi za kufukua shimo hilo kwa kushirikiana na wachimbaji wenzao ili kuokoa maisha yao lakini baada ya kuwafikia walikuwa wameshafariki.

 Ameongeza kuwa baada ya kutoa miili hiyo waliipeleka katika hospitali ya wilaya ya Igunga kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati wakisubiri ndugu wa marehemu kuja kuichukua, alitoa wito kwa wachimbaji wadogo kuwa makini wanapokuwa kwenye shughuli hizo za uchimbaji.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Dk. Merchades Magongo alithibitisha kupokea maiti mbili Mei 26,2021 saa 1 asubuhi.

“Ni kweli tumepokea miili ya watu wawili Mrisho Luge (32) na Mussa Cosmas (41) kutoka kwa Jeshi la Polisi wote wakiwa wamefariki na imeihifadhiwa wakati tunasubiri wanandugu na kufanya uchunguzi kisha tutawakabidhi,” alisema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ACP Safia Jongo amethibitisha kufariki kwa watu hao wawili huku akibainisha chanzo chake kuwa ni ukuta wa shimo la machimbo ulioporomoka na kuwafukia wakati wakichimba madini.

Ametoa wito kwa wachimbaji wote mkoani hapa kuchukua tahadhari wanapokuwa ndani ya mashimo ya machimbo hayo ili kuepusha maafa ya namna hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles