26.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 15, 2021

Dulla Mbabe, Twaha Kiduku shoo Julai 24

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mabondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Twaha Kiduku na Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, rasmi leo Mei 26, 2021 wamesaini mkataba wa kuzichapa Julai 24, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Wanamasumbwi hao wenye upinzani mkubwa mara ya mwisho mwaka jana Uwanja wa Uhuru na Kiduku kushinda kwa pointi.

Pambano linalokuja litakuwa la tatu kwa wababe hao kukutana na limepewa jina la ‘PayBack’, huku Dulla Mbabe akitamba kulipa kisasi siku hiyo.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Dulla Mbabe, amesema mashabiki wa ngumi hataamini kitakachotokea kutokana na alivyojipanga kumuonesha kazi mpinzani wake.

“Makubaliano yamefikia muafaka nipo tayari, atakufa mtu siku hiyo,” amesema Dulla Mbabe.
Naye Twaha Kiduku amesema yeye hana maneno mengi na kuwataka mashabiki wake wasubiri kitakachotokea ulingoni.

” Ndugu zangu mimi nawaomba tukutane tarehe 24, tulieni tu, shoo shoo,” ametamba Twaha Kiduku.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Peaktime Media, , Kapteni Seleman Semunyu, amesema kitendo cha kusaini mkataba kwa mabondia hao ni kuthibitisha kuwa pambano lipo.

Amekuwa lengo kubwa la kuandaa mapambano ni kuinua vipaji na ndiyo sababu siku hiyo kutakuwa na michezo mingi ya utangulizi.

“Naomba wadau wa michezo na wapenzi wa ngumi kuungana na mimi kudhamini pambano hili ili kuwainua vijana na kuendeleza mchezo wa ngumi,” amesema.

Kati ya mapambano 11 yatakayopigwa siku hiyo, baadhi ya michezo mikali itakuwa ni Cosmas Cheka akipigana na Ismail Galiatano kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania(JWTZ), Iddy Pialali atazichapa na Abdallah Luhanja.

Selemani Kidunda(JWTZ) dhidi ya Paul Kamata,George Bwanabucha (JWTZ) atapigana na Sunday Kiwale, huku wanawake Grace Mwakamale(JKT) atazichapa na Happy Daudi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,753FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles