28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mwenezi CCM, Mwenyekiti Mama Ongea na Mwanao wateta

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele maarufu Steve Nyerere, amekutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Shaka Hamdu Shaka leo Jumatano Mei 26 na kuzungumza mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya chama hicho.

Wawili hao wamekutana Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo Mengele ameweka wazi nia ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuhakikisha chama hicho kinasonga mbele kwa kuongeza wanachama huku kikiongozwa kwa weledi.

Shaka amelipongeza Kundi la Mama Ongea na Mwanao ambalo lina mchanganyiko wa wasanii wa filamu na muziki ambapo ameahidi kushirikiana nao kwa kila hatua.

“Kundi hili lina historia na Rais wetu mpendwa Mama Samia kwani tangu alipoanza kugombea kama mgombea mwenza wa hayati John Magufuli, lilijitoa kwa hali na mali na kuzunguka naye nchi nzima kwenye kampeni nami naahidi kushirikiana nanyi bila kusita,” amesema Shaka.

Kwa upande wake Mengele amemuomba Shaka kurekebisha baadhi ya mambo na kukirejesha chama kwenye mstari ikiwamo kuvunja makundi.

“Sisi wasanii tuna imani na wewe kikubwa ni kuondoa matabaka ili chama kirudi kwenye mstari na kuhakikisha Awamu ya Sita chini ya Mwenyekiti Mama Samia Suluhu Hassan kinabaki kwenye weledi wa hali ya juu,” amesema Mengele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles