25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Waasi 6,000 wakamatwa Uturuki

Reccep Teyyip Erdogan
Reccep Teyyip Erdogan

ISTANBUL, UTURUKI

UTAWALA nchini Uturuki umevamia kambi za kijeshi kote hapa nchini na kukamata waasi 6,000 wanaoshukiwa kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyozimwa siku ya Ijumaa.

Katika operesheni kwenye mji ulio magharibi wa Deniel jana kamanda mmoja wa kikosi cha jeshi na zaidi ya wanajeshi 50 walikamatwa.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu serikalini amesema kuwa jeshi limerejesha udhibiti katika asilimia kubwa ya kambi za kijeshi japo kuna baadhi ambazo zipo chini ya usimamizi ya wale waliounga mkono mapinduzi.

Majaji takriban 3000 ambao wanatuhumiwa kupinga Serikali ya Rais Reccep Teyyip Erdogan pia wamesimamishwa kazi.

Rais Erdogan alisema Bunge litaamua iwapo libuni sheria ya hukumu ya kifo au laa kwa waliokula njama za mapinduzi.

Wale waliokamatwa wanatajwa kuwa wafuasi wa kiongozi wa kidini raia wa Uturuki anayeishi Marekani, Fethullah Gulen ambaye analaumiwa kupanga mapinduzi hayo.

Wakati huo huo, Marekani imepinga madai kuwa ilihusika katika jaribio la mapinduzi hayo kutokana na kutajwa kwa Gulen.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema madai kuwa wamehusika na mapinduzi hayo yanasababisha madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao wawili wa Jumuiya ya Kujihami ya Magharibi (NATO).

Aidha Kerry ameutaka utawala nchini Uturuki kuheshimu sheria wakati wa uchunguzi wao kuhusu mapinduzi hayo.

Mapema kupitia hotuba yake, Rais Erdogan alitoa wito kwa Rais wa Marekani Barack Obama kumrejesha Gulen, ambaye amekana kuhusika na tukio hilo.

Marekani inasema kuwa Uturuki ni lazima ithibitishe madai hayo kabla ya uamuzi wa kumkabidhi Gulen kufanyika.

Mapema jana maelfu ya watu walijitokeza wakiimba na kupeperusha bendera ya taifa katika barabara za miji ya Istanbul na Ankara kumuunga mkono Rais Erdogan.

Bustani nyingi mjini Istanbul zilijaa watu waliokuwa wakiimba kuwa ardhi yao na demokrasia haviwezi kuchukuliwa na jeshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles