25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waajiri chanzo cha watumishi kukaimu kwa muda mrefu

Na James Mwanamyoto, Morogoro

Tatizo la Watumishi wa Umma kukaimu nafasi za uongozi kwa muda mrefu bila kupata stahili ya vyeo wanavyokaimishwa, linatokana na waajiri kutozingatia taratibu za kiutumishi pindi wanapowakaimisha watumishi hao kama Waraka wa Utumishi namba mbili wa Mwaka 2018 unavyoelekeza.

Hayo yamesemwa leo De4semba 21, mkoani Morogoro na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) George Mkuchika alipoitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.

Mkuchika amesema, kumekuwa na tabia ya Waajiri wengi hususan katika halmashauri kuwakaimisha watumishi ambao hawana sifa za kukaimu wala kibali cha kukaimu ambacho kinatolewa na Katibu Mkuu Utumishi.

“ili mtumishi aweze kukaimu, anapaswa kuwa na cheo cha Afisa Mwandamizi na kuendelea na pia awe amepatiwa kibali cha kukaimu nafasi husika na Katibu Mkuu- Utumishi ambacho atakitumikia kwa miezi isiyozidi 6 kabla ya kithibitishwa rasmi iwapo atakidhi vigezo vya kukitumikia cheo hicho.

“Kitendo cha Watumishi kukaimishwa bila kufuata taratibu kimekuwa ni chanzo cha malalamiko ya watumishi wengi, hivyo amewataka Waajiri kuzingatia taratibu ili kuepuka malalamiko ambayo yanashusha morali ya utendaji kazi,”amesema Mkuchika.

Wakati huo huo, Mkuchika amewataka Waajiri kuhakikisha wanawawezesha wastaafu kupata mafao yao kwa wakati pindi wanapostaafu ili kuwaondolea usumbufu wa wa kufuatilia mafao yao pindi wanapostaafu ikizingaatiwa kuwa wamelitumikia taifa kwa bidii na uadilifu.

Mkuchika amesema, ili wastaafu wapate mafao kwa wakati, Maafisa Utumishi wanapaswa kufanya maandalizi kwa kukusanya vielelezo vyote vinavyohitajika mapema miezi 6 kabla.

“Kutokana na changamoto hii, nitafanya mkutano na Maafisa Utumishi nchi nzima kama nilivyoahidi hapo awali ili kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu suala hili,” amesisitiza Mkuchika.

Awali, akiwasilisha taarifa ya utekekezaji ya Mkoa wa Morogoro, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo alimwambia, Waziri kuwa, pamoja na mafanikio mazuri yaliyopatikana katika Mkoa wa Morogoro, Ofisi yake ina changamoto ya watumishi kukaimu kwa muda mrefu na wastaafu kutokapata mafao yao kwa wakati pindi wanapostaafu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles