Aslay kupamba Krismas Musoma

0
350

Na Mwandishi Wetu, Musoma

Msanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Aslay’ anatarajia kuwaburudisha wakazi wa mji wa Musoma siku ya Krismas Desemba 25, katika ukumbi wa Le Grand Beach.

Akizungumza na Mtanzaniadigital, Mratibu wa tamasha hilo lililopewa jina la ‘Shangwe za Christmas’, Shomari Binda, amesema maandalizi yote yamekamilika na kilichobaki ni wakazi wa Musoma kusubiri burudani.

“Aslay ameahidi kutoa burudani ya nyimbo zake zote kali na kuwaomba wakazi wa Musoma na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kupata burudani ambayo haijawahi kutokea kabla,” amesema Binda.

Aidha, Binda amesema tamasha hilo litaambatana na muziki wa wa vyombo ‘Live band’ utakaopigwa na bendi ya New Le Grand Band.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here