Shilole azimia baada ya kuvalishwa pete

0
537

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva nchini, Zuweza Mohammed, ‘Shilole’ usiku wa kuamkia leo Desemba 21, amevalishwa Pete na Mchumba wake ambaye pia ni mpiga picha wake maarufu Rommy 3D nakujikuta akizimia.

Tukio hilo limejiri usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Desemba 21, 2020, wakati Shilole alipokuwa akifanya sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Ikumbukwe kuwa, Shilole amevalishwa pete baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Uchebe na sasa amepata mchumba mpya.

Shilole ametumia hafla hiyo kuonyesha gari yake mpya aliyonunua huku akidai kuwa gari hilo amenunua kwa pesa yake na hajahongwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here