27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bashungwa atoa miezi mitatu kwa TaSUBa kujitangaza

Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Bagamoyo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent
Bashungwa ametoa miezi mitatu kuanzia mwezi January 2021 kwa Chuo
cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kujitangaza, kupitia njia mbalimbali
ikiwemo Vyombo vya Habari na Mitandao ya kijamii ili wananchi wakijue
na wajiunge kujifunza Sanaa ambayo ni njia mojawapo ya kujiajiri.

Bashungwa ameyasema hayo leo Desemba 21, 2020 Wilayani
Bagamoyo Mkoa wa Pwani alipotembelea Chuo hicho pamoja na Naibu
wake, Abdallah Ulega na Katibu Mkuu, Dk. Hassan Abbas.

“Tumieni Vyombo vya Habari kutangaza maudhui yanayohusu Chuo hiki, ili muweze kupata wanafunzi wengi ambao watajifunza sanaa,” amesema
Bashungwa.

Waziri huyo amesema, suala la ubunifu katika kutoa elimu ya Sanaa ni
jambo la msingi hivyo ameitaka TaSUBa  kutoa matangazo ya kozi
wanazofundisha  ili kusaidia wasanii na sekta ya Sanaa nchini kuendeshwa
kwa weledi na kuongeza idadi ya vijana katika sanaa.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Abbdalah Ulega ameiagiza TaSUBa kutengeneza filamu ambazo
zinaitangaza nchi yetu ikiwemo historia ya Nchi, Filamu ya Maisha ya Mwalimu  Nyerere, Ushiriki wa Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika ili watanzania  hasa watoto waijue historia ya nchi hii.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dk.Hassan Abbas ameongeza kuwa TaSUBa ni Taasisi kongwe
ambayo iliundwa kimkakati  katika kukuza Sanaa, huku akieleza kuwa
Serikali inaendelea kuwekeza katika Taasisi hiyo ili isaidie katika kuibua
na kukuza vipaji vitakavyojiajiri na kutengeneza fursa kwa wengine.

Vilevile, Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Herbet Makoye amesema katika mwaka
huu wa masomo 2020/2021 chuo hicho kimeongeza udahili wa wanafunzi
ambapo mpaka sasa kimedahili wananfunzi 651 lengo likiwa ni kuzalisha
wataalamu wengi katika fani ya Sanaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles