23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

“Kumuogopa baba ndiyo kumetufikisha hapa”-Jokate

Na Brigiter Masaki, Dar es Salaam

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete leo Jumatatu, Desemba 21 amewaongoza wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuaga mwili wa Urban Costantine Ndunguru ambaye ni Baba Mzazi wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo aliyefariki mwishoni mwa wiki.

Mbali na Kikwete viongozi wengine walioshiriki kwenye ibada hiyo ni pamoja na Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakary Kunambi na wengine.

Awali akizungumza wakati wa ibada hiyo, Joketi amesema walikuwa wakimuogopa sana Baba yao huyo kutokana na ukali aliokuwa nao.

“Baba yetu tulikuwa tunamuogopa sana, alikuwa ni mkali, kipindi pekee ambacho tuliweza kujenga mahusiano nae ni alipokuwa mgonjwa, ugonjwa ulikuja na baraka, alikuwa zaidi nyumbani tukaweza kufahamiana.

“Lakini kumuogopa kule kulitujengea nidhamu ambayo imetufanikisha kufikia malengo yetu na leo kama Watoto tunaweza kumuaga Baba yetu kwa heshima,” amesema Jokate.

Baada ya kuagwa mwili wa Ndunguru umesafirishwa leo kwenda Mbinga Mkoani Ruvuma kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Jumanne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles