28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

VIWANGO VIWABEBE WACHEZAJI USAJILI MSIMU UJAO

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MASHABIKI wa soka watakuwa wameanza kujiandaa na kupendekeza wachezaji wapya watakaofaa kusajiliwa katika klabu zao, kwa kipindi cha usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Usajili wa Tanzania umekuwa ukishangaza kwani mara nyingi wachezaji wamekuwa wakisajiliwa bila kuangaliwa viwango vyao, bali umaarufu wa jina.

Ikiwa zimebaki mechi chache kabla ya msimu huu kufikia ukingoni, tayari baadhi ya viongozi wa timu mbalimbali watakuwa wameanza kutupia macho kuona wachezaji gani wanaweza kuongeza nguvu kwenye vikosi vyao.

Matumaini yetu msimu ujao utakuwa na ushindani zaidi, ikiwa tunalenga mabadiliko mbalimbali ya mpira wa miguu hapa nchini.

Tunatambua jinsi gani viongozi wa  klabu kongwe na nyinginezo katika ligi watakavyojituma kuhakikisha wanamiliki wachezaji wazuri.

Viongozi hawa wamekuwa wakifanya usajili wao kwa mbwembwe nyingi na kutambiana na inapofika wakati wa mchezaji kutoonyesha kiwango walichokitarajia, malalamiko na malumbano hujitokeza.

Lawama nyingi zinaanza kutolewa, lakini hata hivyo makocha wanaofundisha timu wanapata shida ya kumiliki wachezaji wasio na viwango; kwa kifupi wachezaji mizigo.

Wachezaji wasiokuwa na viwango bora huchangia walimu kuonekana hawafai na wengine hufikia hatua ya vibarua vyao kuota nyasi kutokana na timu kushindwa kutimiza malengo iliyojiwekea.

Inapofika kipindi hiki, hutokea sintofahamu baina ya walimu na wachezaji, kwani mwalimu anachotambua ni kuwa mchezaji aliyesajiliwa amekidhi vigezo vyote.

Tujaribu kupiga hatua na kuondoka hapa tulipo, kiwango kiwe sababu sahihi ya wachezaji kujipatia namba katika kikosi na timu husika.

Juhudi za mchezaji zinatakiwa, inafahamika wachezaji  wengi wamekuwa wakiona njia fupi ya kufanikiwa ili warudi kwenye viwango ni kuwakomesha wenzao kwa kuwaroga.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles