25.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

TANESCO ILALA YAANZA KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU

Na NORA DAMIAN
-DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme (Tanesco) Mkoa wa Ilala, limeanza kukata umeme kwa wadaiwa sugu.

Hatua hiyo ya kukata umeme inatokana na agizo la Rais Dk. John Magufuli alilolitoa Machi mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ilala, Athanasius Nangali, alisema wanazidai taasisi za Serikali na watu binafsi lakini taasisi za Serikali zimeonyesha ushirikiano wa kulipa.

 “Taasisi nyingi za Serikali zimeonyesha ushirikiano na tayari tumekusanya Sh bilioni mbili, nyingine tumeingia nazo mkataba ambapo baadhi zimeahidi kulipa mwisho wa mwezi huu,” alisema Nangali.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, taasisi za Serikali zinadaiwa Sh bilioni nne wakati taasisi binafsi zinadaiwa Sh bilioni moja.

Katika operesheni hiyo viwanda vilivyokatiwa umeme ni Kiwanda cha Uchapishaji cha Iprint na kile cha utengenezaji mabomba cha Pipe Industies.

Naye Mhandisi Mdhibiti Mapato Tanesco Mkoa wa Ilala, Daniel Kimambo, alisema Pipe Industries wanadaiwa Sh milioni 29 na Iprint wanadaiwa Sh milioni 16.9.

Alisema viwanda hivyo vimekatiwa umeme kwa sababu madeni hayo ni ya muda mrefu na kwamba zoezi hilo ni endelevu kwa wadaiwa wengine sugu.

Msemaji wa Kampuni ya Pipe, Mohamed Talib, alikiri kampuni hiyo kudaiwa na kuahidi kwenda Tanesco kulipa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,173FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles