24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Vitambulisho vya machinga kuboreshwa, vitumike kwenye mikopo

Ramadhan Hassan -Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Magufuli amesema katika miaka mitano ijayo Serikali  yake inakusudia kuviboresha vitambulisho vya wajasirimali  ili waweze kutambulika benki na hivyo kupata mikopo.

Akizungumza jana wakati akizindua Bunge la 12,Rais Magufuli alisema wakati wa kipindi cha kampeni aliahidi  kwenye miaka mitano ijayo Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali wadogo.

“Kama mnavyofahamu kwenye miaka mitano iliyopita,tulianzisha utaratibu  wa kutoa vitambulisho  maalum kwa wajasiriamali wetu wadogo.

Kwenye miaka mitano ijayo tunakusudia kuviboresha vitambulisho ikiwemo kuweka picha na taarifa nyingine muhimu kama ilivyo kwenye vitambulisho vya Taifa na pasipoti.

“Hii itawezesha wafanyabishara watakaotumia vitambulisho hivyo kutambulika,ikiwemo kwenye benki na hivyo kupata mikopo  kwa ajili ya kukuza biashara.

Alisema hali hiyo itawezesha wafanyabishara wadogo kukuwa kiuchumi  na kutajirika  ambapo alisema hilo  ndio lengo la Serikali.

“Tunataka wafanyabishara wetu wadogo wawe wanakuwa na kutajirika na sio siku zote wabaki  kuwa wafanyabiashara wadogo,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles