24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Virusi vipya yaathiri mamia China

WUHAN, CHINA

WANASAYANSI wameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC kwamba gonjwa jipya lililoibuka nchini China limeathiri mamia tofauti na idadi inayotolewa na maofisa wa serikali nchini humo.

Karibu watu 50 wamethibitishwa kuugua ugonjwa huo unaosababishwa na virusi, lakini wataalamu wa Uingereza wanasema wanakadiria kuwa idadi ya walioathirika inaweza kukaribia 1,700.

Hadi sasa watu wawili wamefariki dunia kwa magonjwa ya kushindwa kupumua, katika jiji la Wuhan mwezi Desemba.

Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko Profesa Neil Ferguson, amesema ana wasiwasi idadi ikawa ni kubwa zaidi.

Singapore na Hong Kong  wamekuwa wakiwachunguza abiria wanaotoka Wuhan na Marekani pia imetangaza kuchukua hatua kama hizo katika viwanja vya San Francisco, Los Angeles na New York.

Taarifa zinaeleza kuwa wakati mlipuko wa ugonjwa huo ukitajwa kuanzia Wuhan, kesi mbili zinazohusu ugonjwa huo zimeripotiwa katika nchi za Thailand  na moja nchini Japan “Hii inasababisha wasiwasi,” alisema Prof. Ferguson.

Aliongeza kuwa: “Wuhan kupeleka kesi tatu katika nchi nyingine inamaanisha kwamba huenda kuna kesi zaidi ambazo hazijaripotiwa.”

Alisema japo inaweza kuwa ni vigumu kupata idadi kamili lakini kutokana na ugonjwa huo kuenea kwa virusi na mazingira ya nchi yenyewe yenye idadi kubwa ya wananchi na idadi ya wasafiri wa ndege hilo linaweza kutoa taswira nini kinaendelea.

Pamoja na hayo Prof. Ferguson alisema ni mapema mno kutangaza hali ya hatari. 

Mamlaka za nchini China zimesema hakuna kesi yeyote ya virusi hivyo kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Badala yake wamesema kuwa virusi hivyo vimetoka kwa wanyama walioathirika kutoka katika soko la vyakula vya baharini na wanyama wa mwituni la Wuhan. 

Taarifa hizi mpya zimekuja ikiwa ni takribani wiki mbili zimepita tangu mamlaka ya China ianzishe utafiti kuchunguza virusi vinavyosababisha ugonjwa huo wa ajabu ambao umewaambukiza watu kadhaa katika mji wa Wuhan.

Ugonjwa huo ulizua hofu mtandaoni na kuhusisha virusi hivyo kuwa unaweza kusababisha kuwa na mtindio wa ubongo na madhara mengine yanayoweza sababisha vifo.

Awali ilidaiwa kuwa kuna uwezekano wa ugonjwa huo kufanana na ugonjwa wa ‘sars’ ambao uliua watu zaidi ya 700 ulimwenguni kote mwaka 2002-03, baada ya kutokea nchini China.

Shirika la Afya duniani la WHO lilisema linaangalia kwa karibu mlipuko huo na itaweza kutoa taarifa zaidi watakapozipata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles