22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Trump aandaa kikosi cha utetezi chenye rekodi kubwa

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump wa Marekani sasa anaonekana kuimarisha kikosi chake cha utetezi wakati kesi inayomkabili itakapoanza kusikilizwa Jumanne ijayo katika Baraza la Seneti.

Trump anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka akituhumiwa kumshinikiza Rais wa Ukraine amchungumze mpinzani wake, Joe Biden wa Democrat ambaye ametangaza kupambana naye kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka huu. 

Wakati kesi yake hiyo ikiwa imefikishwa Baraza la Seneti tayari yeye mwenyewe Trump amekusanya kundi la wanasheria wenye rekodi litakalomtetea.

Kundi hilo linajumuisha majina maarufu kama vile, Ken Starr, Mwendesha Mashtaka ambaye uchunguzi wake miongo miwili iliyopita, ulisababisha kushitakiwa bungeni kwa Rais Bill Clinton aliyekuwa anakabiliwa na kashfa ya ‘Whitewater’. 

‘Whitewater  ni mradi wa ardhi na nyumba ambao familia ya Clinton ilikuwa imewekeza hata hivyo, hawakupatikana na hatia.

Licha ya familia ya Clinton kutopatikana na hatia Kenneth Winston Starr ambaye amezaliwa mwaka 1946 anasifika kwa kufanya chunguzi bora kabisa.

 Ni mwanasheria ambaye amepata kuhudumu katika mfumo wa kimahakama ‘United States circuit judge’  na mwanasheria Mkuu wa 39 Marekani. 

Mbali na Ken Starr, Trump pia amemjumuisha aliyekuwa Profesa wa masuala ya sheria katika Chuo Kikuu cha Havard Alan Dershowitz ambaye amebobea katika sheria za kikatiba na zile zinazohusu uhalilfu.

Dershowitz ambaye ameandika historia nchini Marekani ya kupata u-profesa akiwa na umri mdogo kabisa wa miaka 28, amesema atatoa hoja za kikatiba zinazonuia kumlinda Trump dhidi ya madai kwamba ametumia vibaya mamlaka yake.

Rekodi ya Dershowitz ambaye ameshiriki kesi kadhaa kubwa ni ya juu.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa kama mwanasheria katika kesi za jinai zinazohusu mauaji kati ya 15 alizozisimamia 13 alishinda.

Amewawakilisha watu maarufu kadhaa katika masuala ya kisheria akiwamo Mike Tyson, Patty Hearst na Jim Bakker.

Hatua hiyo, inaongeza uzoefu katika siasa za kushitakiwa rais bungeni pamoja na masuala yanayohusu sheria za kikatiba.

Wengine waliojumuishwa katika kikosi hicho cha utetezi cha Trump ni pamoja na Jeffrey Epstein na O.J Simpson.

Pia wamo Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Frolida Pam Bondi na Robert Ray aliyemrithi Starr kama mshauri binafsi katika uchunguzi wa Whitewater.

Kikosi hicho cha Trump tayari kimeanza kujipanga na wikiendi nzima kimekuwa na shughuli nyingi za kujiandaa kisheria kabla ya kuanza vikao vya kutoa hoja za ufunguzi Jumanne wiki ijayo hata wakati ushahidi ukiendelea kutolewa.

Baraza la Seneti la Bunge la Marekani kwa mara ya tatu katika historia ya nchi hiyo litasikiliza kesi dhidi ya rais, baada ya kupokea rasmi mashtaka mawili Jumatano wiki hii kutoka Baraza la Wawakilishi dhidi ya Rais Donald Trump.

Mashataka hayo yatasomwa Alhamisi mbele ya Baraza la Maseneta 100, ambao baada ya kuapishwa Alhamisi, wanageuka kuwa wajumbe wa baraza la kutoa maamuzi kwenye shauri hilo, wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Marekani John Roberts.

Mashtaka hayo yaliidhinishwa na kutiwa saini na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Nancy Pelosi Jumatano kabla ya kupelekwa mbele ya baraza la Seneti.

Changamoto kubwa hivi sasa ni ikiwa kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti, Mitch McConnell na Warepublikan watakubali madai ya wanademocrats kusikiliza mashahidi muhimu na ushahidi mpya uliojitokeza hivi sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles