22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Van Gaal adai amechoshwa na United

Van GaalMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa Klabu ya Manchester United amedai kwamba hata kama klabu hiyo kuna wakati inafanya vizuri, lakini amechoshwa na mwenendo wake kwa msimu mzima.

Kocha huyo amekuwa na kipindi kigumu msimu huu ambapo uongozi wa klabu hiyo ulikuwa tayari kumfungashia virago vyake lakini ikampa muda, ila kocha huyo bado aridhishwi na mwenendo wa klabu hiyo.

Van Gaal amedai kwamba kuna wakati klabu hiyo inarudi katika ubora wake lakini haichukui muda inaanza kuharibu hivyo inamnyima raha kabisa.

“Kuna wakati timu inatulia na inacheza soka la kisasa, lakini wachezaji wanashindwa kulinda viwango vyao, hivyo ninakosa amani kabisa.

“Kuna michezo ambayo ilinipa furaha sana kama vile dhidi ya Chelsea, nilifurahi japokuwa tulitoka suluhu ila tulicheza soka la hali ya juu.

“Najua kwamba sio kila mchezo lazima tucheze vizuri, lakini inatakiwa kuonesha ubora wetu kwenye michezo mingi, kutokana na hali hiyo mashabiki na viongozi wanakuwa hawatuelewi,” alisema Van Gaal.

Hata hivyo, kocha huyo anaamini kwamba klabu hiyo inaweza kubadilika na kufanya vizuri katika michezo ijayo ya ligi na kuwafurahisha mashabiki wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles