27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Messi: Nipo tayari kuzeekea Barcelona

MessiZURICH, USWISI

MCHEZAJI bora wa dunia wa tuzo ya Ballon d’Or 2015, Lionel Messi, amedai kwamba Barcelona ni sehemu yake sahihi ya kucheza soka hivyo yupo tayari kuzeekea hapo.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Argentina, amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 15 sasa tangu alipoanza soka katika klabu hiyo na hadi sasa amefanikiwa kuchukua uchezaji bora wa dunia mara tano pamoja na mataji mbalimbali.

Juzi alitangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2015 baada ya kuwabwaga wapinzani wake Cristiano Ronaldo na Neymar, katika hafla iliyofanyika mjini Zurich nchini Uswisi.

Kutokana na hali hiyo, Messi amedai kwamba ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa maisha yake ya soka kutokana na mafanikio anayoyapata akiwa na klabu hiyo.

“Nimewahi kuyaongea haya zaidi ya mara 1000 na nitaendelea kuyasema haya kwamba sina mpango wa kuondoka katika klabu hii katika maisha yangu ya soka.

“Lengo langu ni kumaliza soka langu nikiwa nyumbani kwangu, katika maisha ya soka ni Klabu ya Barcelona na ninaamini itakuwa hivyo kama nilivyopanga kwa kuwa klabu hii imenifanya niwe hapa kwa sasa na nionekane kuwa bora duniani,” alisema Messi.

Mkataba wa mchezaji huyo katika klabu ya Barcelona unatarajia kumalizika mwaka 2018, wakati huo mchezaji huyo atakuwa na umri wa miaka 31.

Mchezaji huyo alianza kuitumikia klabu hiyo huku akiwa na umri wa miaka 13, ambapo hadi sasa akiwa na umri wa miaka 28 na kufanikiwa kutwaa mataji mbalimbali kama vile Ligi ya Mabingwa Ulaya, Klabu Bingwa ya Dunia, Ligi Kuu nchini Hispania, Copa del Rey na mengine mengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles