27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Guardiola awaomba radhi makocha England

Pep GuardiolaDOHA, QATAR

KOCHA wa Klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola, amewaomba radhi makocha wa Ligi Kuu nchini England kwa kuwa na wakati mgumu baada ya kusikia kwamba kocha huyo anataka kufundisha timu za ligi hiyo.

Kocha huyo amedai kwamba huu ni msimu wake wa mwisho kuitumikia klabu ya Bayern Munich, hivyo alidai kwamba macho yake ni kufundisha klabu za Ligi Kuu nchini England.

Kutokana na hali hiyo makocha mbalimbali wa nchini England walikuwa na wakati mgumu huku wakiamini kuna uwezekano wa kufukuzwa katika klabu zao na kumpa nafasi kocha huyo.

Makocha ambao walikuwa na wakati mgumu ni pamoja na Manuel Pellegrini wa Manchester City, Van Gaal wa Manchester United, ambapo Guardiola alidaiwa kuwindwa na klabu hizo baada ya kutangaza kwamba anataka kutua England.

“Naomba samahani kwa kuwapa wakati mgumu makocha wa England baada ya kusikia kwamba nataka kufundisha klabu zao huko, najua kuna makocha fikra zao zilikuwa ni kufukuzwa kwa ajili ya ujio wangu, ila naweza kusema nitaweka sawa wapi nitaenda mara baada ya kumaliza mkataba wangu,” alisema Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles