30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Arsenal yapangiwa na Burnlye Kombe la FA

wengerLONDON, ENGLAND

DROO ya raundi ya nne ya michuano ya Kombe la FA, imetoka huku timu za Ligi Kuu nchini England zikipangwa na zile za daraja la kwanza.

Arsenal ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, wao wamepangwa kukipiga na timu ya Burnley, huku Chelsea wao wakiwa ugenini wataanza kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Northampton Town au Mk Dons.

Wakati huo Manchester City wao watakipiga na mshindi wa mchezo kati ya Wycombe Wanderers au Aston Villa, huku majirani zao Manchester United wao watakipiga na Derby County.

West Ham wao watasubiri mshindi wa mchezo utakaowakutanisha kati ya Exeter City dhidi ya majogoo wa Anfield, Liverpool.

Michuano hiyo ya mzunguko wa nne itaanza kutimua vumbi Januari 29 hadi Februari 1 mwaka huu, huku klabu hizo za daraja la kwanza zikionekana kuzitoa jasho klabu kongwe katika michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles