UTORO, MIMBA WAKWAMISHA WANAFUNZI 787 KUHITIMU

0
773

Na SAM BAHARI-SHINYANGA


WANAFUNZI 787, kati ya wanafunzi 4,172 walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2009 hawakuhitimu elimu ya msingi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo utoro na mimba za utotoni.

Licha ya wanafunzi walioandikishwa  mwaka huo, lakini waliosajiliwa kufanya mtihaani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2016, ni 3,385 sawa na asilimia 81.1.

Akitoa taarrifa ya maendeleo ya sekta ya elimu katika kikao cha wadau wa elimu Manispaa ya Shinyanga, Ofisa Elimu Msingi Manispaa hiyo, Yessa Kanyuma alisema wanafunzi 3,385 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kuitimu elimu ya msingi (2016) wavulana  ni 1,826 na wasichana 1,559.

Kanyuma alisema kati ya wanafunzi 3,385 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi 2016 wanafunzi 2,499 wavulana 1,202 na wasichana 1,297 walifaulu na kuchaguliwa kujiunga na shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga sawa na asilimia 74.4.

Alisema kati ya wanafunzi 4,172 walioandikishwa wanafunzi 3,375 sawa na asilimia 99.7 wavulana 1,553, wasichana 1,822, walifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi 2016 ambapo wanafunzi 10 hawakuhitimu sawa na asilimia 0.3

“Takwimu zinaonyesha kuwa mdondoko wa wanafunzi ni mkubwa hivyo inapaswa walimu, wazazi na walezi kuchukua hatua za makusudi ili kupunguza mdondoko wa wanafunzi katika shule za msingi ‘’ alisema Kanyuma.

Mwenyekiti wa kikao cha wadau wa elimu, Josephen Matiro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, alisema walimu watakaosababisha wanafunzi washindwe kujua stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa miaka yote saba wataadhibishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here