KIGOMA WABAINISHA VIFO VYA WAJAWAZITO

0
637

Na EDITHA KARLO-KIGOMA


MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Paul Chawote ameelezwa  kukosekana kwa watumishi wa kutosha katika sekta ya afya mkoani hapa, ndiyo kumechangia ongezeko la vifo vya wajawazito.

Akizungumza juzi kikao cha siku tatu cha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kilichokuwa kikijadili hali ya vifo vya wajawazito mkoani Kigoma, Dk. Chawote alisema wanao upungufu wa asilimia 65 ya watumishi wanaotakiwa kutoa huduma kwa wananchi hali inayochangia vifo vya akina mama wajawazito kuongezeka.

Alisema wastani daktari mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwa 10,000 hadi 15,000, lakini mkoa huo, anahudumia wagonjwa 40,000 hadi 50,000 kwa mwaka hali ambayo alieleza inatokana na uhaba wa watumishi wa kada hiyo.

Alisema kutokana na hali hiyo,  vifo vya  wajawazito vimeongezeka kutoka 68 mwaka 2015 hadi 96 mwaka jana.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Anna Kalinda alisema wajawazito wamekuwa wanajifungulia nyumbani na kufariki  dunia.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Palangyo aliwaambia wadau mbalimbali wa afya kuwa, Serikali itaendekea kuboresha utoaji wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi ili mikakati waliyoiweka iweze kutekelezeka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here