USILOLIJUA KUHUSU WANYAMA: TEMBO HULA KILO 150 ZA MAJANI

0
1649

TEMBO HULA KILO 150 ZA MAJANI


TEMBO ni mnyama aishie mbugani, ndiye mnyama mkubwa kuliko wanyama wote katika uso wa dunia. Mnyama huyu ni mrefu, mnene na ana wastani wa kilo zaidi ya 3000, mbali na uzito huo lakini ana urefu wa futi 13 ni kimo kikubwa. Miguu yake ya mbele ni mirefu kidogo kwa miguu ya nyuma, mnyama huyu hula majani, mizizi, matunda n.k. Chakula chake hutokana na mimea tu, ambapo chakula chake ni kilo zipatazo 150 za majani.

 

Kichwani kwake ana viungo vyote alivyonavyo mwanadamu, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya viuongo vyake huwa havionekani kwa urahisi. Mfano watu wengi huwa hawajui mdomo wa tembo upo eneo gani na wanaoweza kukuonesha mdomo wanaweza shindwa kabisa kuonesha pua ya tembo ilipo, masikio yake ni makubwa kiasi kwamba hufunika sehemu kubwa ya kichwa na eneo kidogo la mgongo huguswa.

 

Tembo ndio mnyama ambaye ana kichwa kikubwa, ambapo ndani ya kichwa chake kuna sehemu kubwa iliyobeba ubongo wake. Tembo wa Afrika ndio wakubwa na wenye mvuto, hubeba mimba kwa miezi 22 yaani mwaka mmoja na miezi kumi, baada ya hapo huzaa mtoto mmoja au wawili. Watoto wa tembo huzaliwa wakiwa na kilo zaidi ya 100.

Katika mbuga za wanyama tembo ndio kiumbe pekee ambaye hawindwi na mnyama yeyote, isipokuwa watoto wake tu, lakini kwa bahati mbaya adui yake mkubwa ni jangiri yaani binadamu na kinachomponza ni meno yake ambayo kwa lugha nyingine huitwa pembe.

Upana wa ngozi yake ni zaidi ya nchi moja, ndio maana hata wawindaji haramu hutumia silaha nzito kuwawinda na hata anapokufa mzoga wake huwapa tabu wanyawa wanaokula nyama kumtafuna.

Tembo ni mnyama anayeamini katika amani, lakini ni mtata anapohisi kuwa unataka kumdhuru hata kama yeye ndiye aliyekukosea, katika hili unaweza kuona mfano pindi wanapovamia mashamba ya wakulima na kufanya uharibifu wa mazao, inapotokea wakulima wakaonekana tu, tembo hutambua usalama wao upo shakani hivyo wao ndio huanza kufanya fujo ambazo si rahisi kwa binadamu kuhimiri. Huua vibaya kwa kuwa hutumia miguu yake mizito kukukanyaga pindi anapomdondosha kiumbe anayeamini ni adui kwa wakati huo, madhira haya huwapata zaidi  wakulima ambao mashamba yao huvamiwa na mnyama huyu, hasa wakulima ambao hutaka kujaribu kuwaswaga watoke mashambani.

Tembo ni miongoni mwa wanyama ambao wanaishi kwa muda mrefu, hata binadamu anaweza akaachwa kwa miaka ambayo tembo huishi, wanyama hawa hudumu kwa miaka 50 hadi 80. Pamoja na hayo yote wanyama wanyonge huamini kukaa naye jirani kwa sababu inakuwa ni ngumu kuwindwa kwani hapendi kushtuliwa na kupigiwa kelele.

Wiki ijayo tutaangalia sifa za mnyama huyu. Pia unaweza kupendekeza mnyama unayetaka tumzungumziekupitia namba 0715202047.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here