DIAMOND: HAMISA JITOKEZE, MTAJE MWENYE MIMBA

0
1386

Na ESTHER GEORGE


MSANII mkali wa Afrika Mashariki, Nassib Abdul (Diamond Platinum), amemtaka mrembo Hamisa Mobeto aibuke na kumtaja mwenye mimba inayodaiwa anayo.

Mkali huyo wa muziki alidai hakuwahi kutoka na mrembo huyo aliyetamba kwenye video za nyimbo mbalimbali za bongo fleva, huku akimtaka ajitokeze aweke wazi huo ujauzito wa nani ili maneno yaishe.

“Utata ulianza kwenye video ya Salome ambapo Hamisa alicheza watu wakatunga mengi ila mimi sijawahi kutoka naye na inaweza kumpa wasiwasi mpenzi wake, lakini naye si ajitokeze aseme nani mwenye mimba,” alisema Diamond.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here