22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Upanuzi chujio la maji Geita wafikia asilimia 90

Na Yohana Shida, Geita

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Geita (GEUWASA) imebainisha kuwa mradi wa upanuzi wa chujio la maji Nyakanga umefikia asilimia 90 na mradi unaendelea ili kuweza kukamilisha kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Geuwasa, Mhandisi Frank Chang’awa amesema hayo katika viwanja vya maonyesho sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini mjini Geita.

Amesema mradi huo unaotekelezwa kwa thamani ya Sh bilioni 1.1 unatarajiwa kupunguza changamoto ya mgawo wa maji mjini Geita kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita laki mbili hadi lita laki 3.5 kwa saa.

Aliongeza, upanuzi wa chujio hilo unafanyika katika chanzo kikuu cha maji mjini Geita ambapo kwa sasa uwezo wake ni kuzalisha wastani wa lita milioni nne kwa siku ikilinganishwa na mahitaji ya lita milioni 18 kwa siku.

Alisema, pia uzalishaji wa maji kwa siku utaongezeka kutoka milioni nne mpaka milioni saba na kuongeza masaa ya upatikanaji wa huduma kutoka masaa 14 mpaka masaa 18-20 kwa siku kwenye mtandao wa maji.

“Tuna Miradi mbalimbali ya Mpango wa Mda Mfupi ya kuongeza upatikanaji wa Maji, kwani tupo asilimia 75 na huduma ya Maji inatoka kwa Masaa 14 kwa wastani Badala ya Masaa 20 maana yake kuna maeneo mengi yanapata maji kwa Mgao,” amesema Mhandisi Chang’awa

Mhandisi Chang’awa amesema wamejipanga kuhakikisha wananchi wa Mji wa Geita wanapata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 100 ili kukuza kasi ya Uchumi ndani ya Mji wa Geita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles