28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

UONGOZI WA KITUO CHA LEVOLOSI KUNG’OLEWA

NA MWANDISHI WETU


waziri-mkuu-kassim-majaliwaWAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Frida Mokiti  kubadilisha uongozi wa  Kituo cha Afya cha Levolosi baada ya kulalamikiwa kutoa huduma mbovu kwa wajawazito.

Pia amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kujenga hospitali za wilaya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana alipotembelea  Hospitali ya Mkoa ya Mount  Meru, ambapo alisema
tatizo la msongamano wa wagonjwa hospitali za rufaa na hospitali nyingine ni lazima lipatiwe ufunguzi.

“Hatuhitaji kuwa na madaktari ambao wanasumbua wagonjwa. Daktari wa Mkoa hakikisha kile kinacholalamikiwa kule Levolosi kinatafutiwa ufumbuzi.

“Hapa Mount Meru hakikisheni mnaboresha mazingira ya vyoo kwenye wadi  za wazazi pamoja na kujenga sehemu ya kuoshea vyombo kwa wagonjwa, ” alisema.

Awali alipotembelea wodi ya kinamama wanaosubiri kujifungua, mmoja wa wagonjwa, Glory Paul Mkazi wa Olasiti alimweleza Waziri Mkuu kuwa mtoto wake alifia tumboni baada ya wauguzi na  madaktari wa kituo cha Afya cha Levolosi  kuchelewa kumpatia matibabu.

“Wakati nahudhuria kliniki nilishaambiwa na daktari kuwa natakiwa kujifungua kwa njia ya upasuaji na siwezi kujifungua kwa njia ya kawaida, nilimwambia nesi kuwa  natakiwa kufanyiwa upasuaji wakanikatalia na kunilazimisha nijifungue kwa njia ya kawaida ambapo ilishindikana na baada ya muda waliniambia kuwa mtoto amekufa na wananifanyia upasuaji ili kuokoa maisha yangu,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alisema amepokea maagizo ya Waziri Mkuu, ambayo yanalenga kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kusisitiza kuwa awali alichukua hatua za kinidhamu kwa watoa huduma za afya kituoni hapo na ataendelea kusimamia nidhamu ya kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi juu ya huduma za afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles