30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

HALMASHAURI ZAPIGWA ‘STOP’ KUPIMA VIWANJA

NA ELIUD NGONDO, SONGWE


angelina-mabulaNAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba, Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, ameziagiza halmashauri zote nchi kuacha mara moja kupima viwanja bila kuwashirikisha wananchi.

Kauli hiyo aliitoa jana wilayani Mbozi mkoani Songwe wakati wa ziara yake ambapo Mabula alisema migogoro mingi ya ardhi inatokana na kutowafidia wananchi ambao ndio waliokuwa wakiyatumia tangu miaka ya nyuma.

Alisema wananchi wanapaswa kuingizwa kwenye miradi ya viwanja na anatakiwa kupewa kipaumbele cha kwanza kupimiwa kiwanja chake cha kujenga kabla ya halmashauri kuchukua jukumu la kuviuza.

“Mwananchi atapatiwa viwanja kwa matakwa yake na yeye ndiye atakayeamua kulipwa fidia au kupewa kiwanja kilicho pimwa ili kuweza kuondokana na migogoro hii isiyokuwa ya lazima,” alisema Mabula.

Mabula alisema asilimia kubwa ya kero za  wananchi ni juu ya migogora ya ardhi ambayo imekuwa ikitokana na kuuzwa viwanja vyao na halmashauri bila kuwepo utaratibu na ushirikishwaji na wananchi kuendelea kuichukua Serikali yao.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliozungumza na MTANZANIA walisema maagizo ya naibu waziri huyo yanatakiwa kusimamiwa na kutekelezwa kutokana na kuwepo tabia ya halmashauri kupuuza na kuanza kuuza viwanja hivyo.

Amos Simwinga Mkazi wa Mbozi alisema wananchi wamekuwa wakichukuliwa viwanja vyao kwa madai ya kuwa watalipwa fidia na halmashauri hizo lakini hakuna lolote linalotekelezwa.

Alisema kumekuwepo na uporaji wa haki za wananchi hali ambayo inasababisha Serikali kuanza kuchukiwa kutokana na halmashauri hizo kutumia vibaya mamlaka zilizonazo na kunyang’anya viwanja vya wanyonge kisha kuwauzia matajiri.

Hakim Msongole alisema agizo hilo kama litasimamiwa kikamilifu wananchi watakuwa ndio wa kwanza kutoa maeneo yao kupimwa na kupewa fidia zao kuliko ilivyo kuwa awali walipokuwa wakichukuliwa maeneo hayo bila kuwepo fidia zao.

“Lawama kubwa ni kwa hawa maofisa ardhi ambao unakuta anaingia kwenye viwanja vya watu na kuanza kupima baada ya siku chache unakuta mtu tajili anakuja kujenga wakati wewe mmiliki haujaambiwa chochote na fidia yako hujapewa,” alisema Msongole.

Alisema hali hiyo ndiyo imekuwa chanzo cha migogoro mingi nchini kuhusu idara ya ardhi kwa kufanya mambo kinyume na taratibu zinavyotakiwa na wananchi waendelee kunufaika kwa kujenga nyumba au kuyauza maeneo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles