23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

United imechapwa, Ronaldo rekodi kibao

JANA Cristiano Ronaldo alifunga bao moja lakini halikutosha kuinasua Manchester United katika kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Young Boys, mtanange wa hatua ya Ligi ya Makundi uliochezwa nchini Uswis.

Licha ya Mashetani Wekundu kudondosha pointi tatu, hili lilikuwa ni bao la 135 kwa Ronaldo tangu aanze kucheza michuano hiyo, akipachika 16 akiwa na ‘uzi’ wa Man United.

Aidha, takwimu zinazonesha kuwa kadiri umri unavyosonga, ndivyo Mreno huyo anavyozidi kuwa bora kwenye ishu ya upachikaji mabao. Ndiyo, bao la jana lilikuwa la 68 kwenye Ligi ya Mabingwa tangu alipofikisha umri wa miaka 30.

Kama hiyo haitoshi, Ronaldo sasa ameifikia rasmi rekodi ya Lionel Messi. Kabla ya jana, Messi ndiye aliyekuwa mchezaji aliyezifunga timu nyingi (36) kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa.

Bao la jana likamfanya Ronaldo awe amefunga katika misimu yote 16 ya hivi karibuni, jambo lililowahi kufanywa na mastaa wawili tu; Karim Benzema na Messi.

Mwisho, mechi ya jana ilikuwa ya 177 kwa Ronaldo, hivyo kuifikia rekodi ya kia Iker Casillas aliyekwua akishikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mara nyingi katika historia ya Ligi ya Mabingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles