24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri DRC atoka gerezani

ALIYEKUWA Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Dk. Eteni Longondo, ameachiwa huru baada ya siku 17 alizokaa katika gerezani kuu la Kinshasa.

Longondo, ambaye alikamatwa kwa tuhuma za kutumbua Dola za Marekani milioni sita (zaidi ya Sh bil. 13 za Tanzania) zilizotengwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya Corona, ameachiwa kwa dhamana.

Haijawekwa wazi kama mashitaka yake yataanza kusikilizwa tena lakini mshirika huyo wa Rais Felix Tshisekedi anafahamu kile kilichomkuta mtangulizi wake kwenye Wizara ya Afya, Dk. Oly Ilunga.

Baada ya kukutwa na hatia alipokuwa akishitakiwa kwa tuhuma za ‘upigaji’ wa fedha za kukabiliana na Ebola, Dk. Ilunga alihukumiwa kifungo cha miaka mitano na anaendelea kusota gerezani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles