26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Taliban waanza kutibuana

IMERIPOTIWA kuwa umetokea mgogoro mkubwa ndani ya Ikulu ya Afghanistan baada ya viongozi wa Serikali mpya ya Taliban kukorofishana, kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Kwa kile kilichoripotiwa na BBC kikitokana na chanzo kilichopo ndani ya Taliban, mvutano umezuka baada ya kila kiongozi kujiona ndiye aliyefanikisha mpango wa kuiondoa Marekani nchini humo.

Juu ya mvutano unaoendelea, chanzo kilichohojiwa na BBC kimedai kiongozi mwandamizi, Mullah Abdul Ghani Baradar, alitupiana maneno na Waziri wa Wakimbizi, Khalil ur-Rahman Haqqani.

Wawili hao wanatofautiana kimtazamo, ambapo Baradar anaamini ushindi dhidi ya Marekani ulitokana na namna alivyosimamia diplomasia, ikiwamo kuzungumza na utawala wa Rais Donald Trump. Lakini sasa, Haqqani haoni kama diplomasia ilifanikisha ushindi wa Taliban na badala yake anaona ni mapigano aliyoongoza ndiyo yaliyosababisha Kundi hilo liingie madarakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles