23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Maguire, Solskjaer: Refa amezingua

NAHODHA wa Manchester United, Harry Maguire, na kocha wake, Ole Gunnar Solskjaer, wanaamini haikuwa sahihi kwa mwamuzi kumlima kadi nyekundu beki wa pembeni, Aaron Wan-Bissaka.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa, Man United wakiwa ugenini nchini Uswis, waliifunga Young Boys mabao 2-1 na Wan-Bissaka alipewa ‘umeme’ kipindi cha kwanza baada ya kumchezea rafu Christopher Martins.

Cristiano Ronaldo aliitanguliza Man United dakika ya 13 lakini Moumi Ngamaleu aliisawazishia Young Boys, kabla ya Theoson-Jordan Siebatcheu naye kuwafungia wenyeji.

Kwa upande mwingine, Maguire amesisitiza kuwa hakuna mchezaji anayemlaumu Jesse Lingard baada ya pasi yake kunaswa na Siebatcheu aliyefunga bao la ushindi. “Inasikitisha lakini ndiyo soka, ni kawaida watu kufanya makosa,” amesema Maguire.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles