28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa Museveni: Watakaojaribu kupindua Serikali watakiona

MTOTO wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema itachukua saa chache tu kuwabaini na kuwaadabisha wale watakaojaribu walau kufikiria kupindua Serikali kama ilivyotokea nchini Guinea.

Siku chache zilizopita, jeshi la Guinea likiongozwa na Luteni Mamady Doumbouya lilishika dola kwa kuiweka kando Serikali ya Rais Alpha Conde.

Kwa upande wake, mtoto wa Rais Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema jaribio la kupindua Serikali halifanikiwa nchini Uganda na kama litatokea basi litazimwa ndani ya muda mfupi.

Kauli ya Luteni Jenerali huyo inatanguliwa na kile alichokifanya baba yake, Rais Museveni, ambapo wiki iliyopita alilaani vikali mapinduzi ya Guinea akisema ni jambo lisilokubalika.

Licha ya kupingwa vikali na jumuhiya za kimataifa, hatua hiyo ya jeshi imepokewa kwa mikono miwili na raia wa Guinea waliokiri kufurahishwa na kuondoshwa madarakani kwa Rais Conde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles