25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Ukame wa mabao Ligi Kuu wamtesa Kagere

ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KINARA wa mabao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Meddie Kagere ameweka wazi kuwa, anapata mateso makubwa ya nafsi kutokana na kushindwa kuongeza idadi ya mabao aliyonayo kwa sasa.

Kagere amecheza michezo minne kati ya mitano ya Simba, tangu kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kusimama Machi 17 mwaka huu kutokana na janga na corona.

Hata hivyo, katika michezo hiyo hajafanikiwa kufunga bao lolote kwani mara ya mwisho kutikisa nyavu ilikuwa kabla ya ligi hiyo kusimama ambapo  Simba ilishinda mabao 7-0, huku yeye akifunga manne.

Lakini tangu kuanza kwa msimu huu, Kagere amefanikiwa kufunga mabao 19 na kuweka bayana kuwa lengo ni kufikisha 30.

Akizungumza na MTANZANIA ,Kagere alisema Simba amekuwa akiumizwa na hali hiyo ya kucheza bila kufunga mabao kwakua ndiyo jukumu lake la msingi.

“Sijakata tamaa ya kufikisha malengo yangu kwa sababu mechi bado tunazo, lakini kukosa kufunga katika michezo mitano mfululizo kwangu ni maumivu.

“Kulingana na nafasi ninayocheza, jukumu langu kubwa ni kufunga, kushindwa kufanya hivyo ni kosa ambalo napaswa kulisawazisha kwa namna yoyote ile,”alisema Kagere ambaye ni raia wa Rwanda.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles