Irene Uwoya awajia juu wanaomsema vibaya

0
270

GLORY MLAY

MSANII wa filamu hapa nchini, Irene Uwoya, amesema kuwa, watu wengi wanamshangaa kuwa na maneno mabaya na kusahau wao ndio waliomfundisha.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Irene alisema kuwa, kawaida yake yeye si muongeaji kwasababu hapendelei kufuatilia mambo ya watu, ila wao wanamchokoza kitu ambacho hakifurahii.

“Watu wengi wananishanga sana siku hizi, wanasema nimekuwa na maneno. Ukweli ni kwamba wamenifundisha wao kuongea maana nilikuwa sina tabia ya maneno na mtu kabisa, lakini wananitafuta kama wanajua ukoo wangu, inaumiza sana,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here